Hassan Mwakinyo "Ningembonda Yule Mzungu Ningekuwa Nimeuaga Umaskini"


Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amelizungumzia pambano lake alilopoteza raundi ya 4 kwa TKO dhidi ya Bondia Liam Smith wa Uingereza, Septemba 04, 2022. Mwakinyo amesema ilimuumiza lakini haijamkatisha tamaa.

Akimueleza mtangazaji Millard Ayo kwenye kipindi cha Amplifaya cha Clouds Fm, Mwakinyo amesema pambano lake na Liam Smith lilikuwa na nafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake na kumuondoa katika umasikini.

”Nimekosa hela nyingi sana kutokushinda lile pambano, lakini sijawahi kukata tamaa na silaumu mipango ya Mungu. Ningeweza kuuaga umasikini. Ningeweza kukodisha bodaboda wote wa Tanga, kila mmoja ningempa bajaji tano halafu angekuwa ananirudishia hela kwa namna anayotaka mwenyewe.” ameeleza Hassan Mwakinyo.

Mwakinyo pia ameongeza kwamba endapo angekuwa ameshinda kwenye lile pambano, ilikuwa ni nafasi ya kumsogezea mkataba wa pambano jingine la pesa ndefu zaidi.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad