Lulu Michael Ajibu Kuhusu Kumfuatilia Mumewe Majizzo


Kama unadhani staa wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu anatabia ya kumfuatilia mumewe kama ana mwanamke mwingine (michepuko) basi unajidanganya! Ametoa jibu kuhusu hilo na sababu juu.

Shabiki mmoja alimua kumuuliza swali hilo Lulu akichati na mashabiki wake kupitia insta story, kufuatia kutokea kwa habari kubwa iliyogonga vichwa vya habari mwanzoni mwa wiki hii, habari kuhusu mume na mke uliyotokea huko Nigeria ambapo mke wa ndoa alifariki Dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari akimfuatilia kwa kumfukuzia mumewe ambae alikuwa kwenye gari lingine na mwanamke ambae imeripotiwa kuwa ni mchepuko wake.

@elizabethmichaelofficial ambaye ni mke wa Majizzo (Boss wa kituo cha Radio na TV cha E) amejibu hivi; "Watu wangu wa karibu wananijua, mimi mwenyewe kuna muda sijifuatilii... Na kutofuatilia sio kwamba hujali. Ni kuchagua kuwa upande chanya ya kuepeusha matatizo yasiyo na suluhu."

"Yani ukifuatilia hakikisha utakacho kutana nacho unajua namna ya kutatua. La sivyo unakuwa umeongeza shida juu ya shida." - ameeleza Lulu katika ujumbe wake kupitia Insta Story yake.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad