Makocha hawa wamekalia moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



IKIWA Ligi Kuu imesimama kwa muda kupisha kalenda ya kimataifa ikiwamo kufuzu kwa fainali ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan), kazi na mtihani upo kwa baadhi ya makocha wakiwamo waliotua nchini msimu huu.

Juzi, uongozi wa Azam FC ulitangaza kuachana na kocha mkuu, Abdi Hamid Moallin na msaidizi wake, Omary Nasser baada ya mechi mbili.

Ligi Kuu inatarajia kuendelea Septemba 6 kwa mechi kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti, ambapo itashuhudiwa kila timu ikipambana kusaka alama tatu ili kujiweka pazuri katika msimamo. Vita ya kuwania ubingwa, nafasi nne za juu na kukwepa kushuka daraja itakuwa ni kampeni maalumu ya kila timu katika kujihakikishia mafanikio msimu huu pengine zaidi ya msimu uliopita.

Katika msimu uliopita Yanga ilitwaa ubingwa huku ikiweka rekodi tamu ya kumaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote, lakini wakifanya umafia kwa watani zao Simba kwa kuchukua makombe yote mikononi mwao ikiwamo Ngao ya Jamii.


Pia mbali na Yanga, zipo timu nyingine zilizoonesha uwezo na kuandika rekodi ya kwanza ikiwamo Geita Gold waliomaliza nafasi nne za juu na sasa watashiriki kombe la shirikisho Afrika, huku Coastal Union nao wakiingia kwenye heshima mpya ya kufika fainali ya ASFC.

Mwanaspoti limeangalia makocha wote wa Ligi Kuu ukiachana na Moallin aliyetimuliwa ambao kwa namna fulani watakuwa na kibarua kizito kufikia malengo ya klabu zao na vinginevyo wanaweza wakajikuta wakiishia njiani pale matokeo yatakapokuwa mazito.

Masoud Djuma - Dodoma Jiji

Kocha huyo raia wa Burundi hajaanza msimu vizuri baada ya kupoteza mechi mbili alizosimamia katika Ligi Kuu licha ya usajili imara alioufanya msimu huu.


Djuma ambaye aliwahi kuinoa Simba, ndiye kocha mkuu wa Dodoma Jiji ambapo katika mechi mbili zilizochezwa amepoteza zote, lakini wakiruhusu idadi kubwa ya mabao (matano) wakifunga mawili. Iwapo hali itaendelea kuwa hivyo, huenda mabosi wakamuonyesha njia ya kutokea kwani itakuwa hajafikia malengo yao tangu alipotua msimu uliopita kuchukua mikoba ya Mbwana Makata aliyetemwa.

Joselin Sharif - Polisi Tanzania

Bado hajaonyesha kitu kipya katika kikosi cha maafande hao, ambao walimtoa Burundi kuja kuziba pengo la Malale Hamsini.

Sharif alitua msimu huu kikosini humo ambapo katika michezo miwili kwake hajashinda hata mmoja, akipoteza na kutoa sare tu, matokeo ambayo kiuhalisia yanamuweka kwenye presha. Ikumbukwe Polisi Tanzania pamoja na kumaliza salama msimu uliopita, lakini ilikuwa miongoni mwa timu zilizopitia wakati mgumu hadi kumfanya aliyekuwa kocha, Malale kumwaga chozi katika moja ya mechi.

Abdallah Mubiru - Mbeya City

Ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya kazi hapa nchini, Mubiru anakumbana na wakati mgumu katika kuihakikishia Mbeya City kuendelea kubaki Ligi Kuu lakini kuio-ngezea heshima aliyoikuta ya msimu uliopita.


M-beya City ikiwa chini ya kocha Mathias Lule msimu uliopita iliweka heshima ya kipekee kwa kuwa timu iliyochukua pointi nyingi (tisa) kwa vigogo wa soka nchini, Simba, Yanga na Azam.

Pia Mbeya City haijawahi kushuka daraja tangu ilipopanda Ligi Kuu msimu wa 10 sasa, hivyo atapaswa kuonyesha uwezo na ufanisi wake kwa chama hilo lenye mashabiki wengi jijini Mbeya, vinginevyo anaweza kujikuta akirudi kwao Uganda.

Fred Felix ‘Minziro’ - Geita Gold

Msimu uliopita Minziro alikuwa miongoni mwa makocha walioweka rekodi na heshima kwa timu zao, alipoaminiwa kwa kukabidhiwa majuku makubwa kuiongoza Geita Gold. Ikumbukwe timu hiyo ikiwa ndio mara ya kwanza kucheza Ligi Kuu, ilikuwa chini ya Ettiene Ndayiragije ambaye hakuweza kudumu zaidi ya mechi nne na kujikuta akifungashiwa virago kufuatia matokeo yasiyoridhisha.

Minziro aliweza kumudu vyema kazi yake kwa kuifanya Geita Gold kuwa timu tishio ilipomaliza nafasi nne za juu na sasa inajiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.


M-simu huu timu hiyo haijaanza vyema kutokana na matokeo waliyopata, ambapo kati ya michezo miwili imeambulia alama moja tu ilipotoa sare ya 1-1 na Azam FC huku ikinyukwa na Simba 3-0.

Kocha huyo na mwenzake, Mathias Wandiba watakuwa na kazi ngumu kuwahakikishia mashabiki kuwa msimu uliopita hawakubahatisha kwa kuipa matokeo mazuri mashindano yote.

Zoran Maki - Simba

Pamoja na kuanza kwa moto mkali Ligi Kuu kwa kushinda mechi zote mbili na kukaa usukani, lakini Kocha wa Simba Zoran Maki bado ana kibarua kigumu kutetea nafasi yake kwa Wekundu. Hatua ya kufungwa na watani zao, Yanga 2-1 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii iliwatonesha kidonda mabosi na hata mashabiki ambao walihitaji kulipa kisasi kwa wapinzani hao.

Hata hivyo bado mashabiki ni kama hawajamkubali sana Kocha huyo wakilaumu kupoteza taji la kwanza, huku matumaini yakibaki kwenye Ligi Kuu na kombe la shirikisho (ASFC) wakitaka kuyarudisha Msimbazi.

Simba ilimpa mkataba wa mwaka mmoja Kocha huyo, ambapo pamoja na mambo mengine walihitaji kurejesha makombe yote ambayo msimu uliopita walikosa, hali ambayo inamuweka kwenye presha kubwa.


Pia timu hiyo ina kabiliwa na mashindano kadhaa ya ndani na nje ya nchini ikiwamo Klabu bingwa Afrika, hivyo atapaswa kusuka kikosi vziuri cha kumpa matokeo mazuri na kuendelea kupata ugali msimbazi tofauti na hapo atajikuta akirudi kwao.

Zuberi Katwila  -  Ihefu

Miongoni mwa makocha ambao hawapati usingizi mzuri ni pamoja na Katwila ambaye amekutana na kisiki Ligi Kuu kwa kuanza na vichapo mfululizo. Ihefu imerejea Ligi Kuu baada ya msimu uliopita kushiriki Championship huku ikipanda na mzuka mwingi kwa kusajili mastaa kadhaa waliowahi kutamba na timu kubwa za Simba, Yanga na Azam.

Hata hivyo pamoja na kikosi alichonacho Katwila, lakini hali imekuwa ngumu sana hali ambayo inamfanya kufikiria vingivyo kwani baada ya kushuka nayo ameweza kupanda nayo tena.

Iwapo atafululiza michezo mingine mitatu mbeleni bila ushindi, huwenda akajikuta akichati nje ya grupu la Ihefu kwani mabosi wake watashindwa kuvumilia kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya.

Patrick Odhiambo  -  Tanzania Prisons

Msimu uliopita presha ilikuwa kubwa kwa Odhiambo kutokana kile alichopitia kuinusuru timu kubaki Ligi Kuu.

Hali ilikuwa tete sana kwake hadi alipojihakikishia kubaki salama kupitia mtoano hatua ya pili kwa kuwafunga JKT Tanzania ya Championship 2-1. Kwa sasa kocha huyo ambaye ameanza na pointi tatu kati ya mechi mbili alizosimamia, atakuwa na kazi nzito kutoruhusu mapigo ya moyo kurudia.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad