Mayele, Morrison waliamsha Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



YANGA juzi ilirudi mazoezini na kasi kubwa baada ya wachezaji kupewa mapumziko ya siku tatu wakitoka kumpiga mtu jumla ya mabao 9-0, lakini habari nzuri kwa wanayanga ni kurejea kwa mastaa wawili walioibua hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kuwa majeruhi, Bernard Morrison ‘BM33’ na Fiston Mayele.
YANGA juzi ilirudi mazoezini na kasi kubwa baada ya wachezaji kupewa mapumziko ya siku tatu wakitoka kumpiga mtu jumla ya mabao 9-0, lakini habari nzuri kwa wanayanga ni kurejea kwa mastaa wawili walioibua hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kuwa majeruhi, Bernard Morrison ‘BM33’ na Fiston Mayele.

Morrison alikosa mechi mbili za kimataifa ambazo Yanga ilicheza na Zalan na kuifunga nje ndani kwa mabao 4-0 na 5-0 sambamba na ile ya Ligi Kuu Bara waliyoipasua Mtibwa Sugar 3-0, wakati Mayele alitoka uwanjani akichechemea baada ya kutupia hat-trick ya pili akiwazamisha mabingwa hao wa Sudan Kusini.

Hata hivyo, mastaa hao juzi walikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichojifua kwenye ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam kuonyesha mambo kwao yapo freshi.

Iko hivi. Yanga juzi ilirudi kazini ikianzia gym ambapo ilijifua kwa saa mbili chini ya kocha msaidizi, Cedric Kaze ambaye naye alishiriki kwa kukimbia sawa na wachezaji kwa baadhi ya mazoezi na kocha wa viungo Helmy Gueldich, raia wa Tunisia.


Kazi hiyo ikaendelea jana asubuhi dozi ikipandishwa ikianzia ufukweni ambapo mastaa hao walitumia tena saa mbili pale Coco wakipiga kazi nzito kwa mazoezi tofauti ya kujenga pumzi na stamina ya mwili, huku Mayele na BM33 wakiliamsha sambamba na wenzao mwanzo mwisho.

Kitu kilichowavutia mashabiki wa timu hiyo ambao waliangalia mazoezi hayo ni kurejea kwa Mayele ambaye alishtua baada ya kupata maumivu katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na Mayele pia Morrison naye alikuwa mzigoni akipiga kazi sawasawa na wenzake baada ya kukosa mechi tatu baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mchezo wa sare ya mabao 2-2 wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam.


Yanga ilikuwa na wachezaji 17 katika mazoezi hayo wakiwemo Yannick Bangala, Mayele, Joyce Lomalisa, Zawadi Mauya, Gael Bigirimana, Yusuf Athuman, Salum Abubakar ‘Sure boy, Morrison na Djuma Shaban, Heritier Makambo, Tuisila Kisinda, Bakari Mwamnyeto na Eric Johola.

Wengine ni; Dickson Ambundo, Jesus Moloko, Farid Mussa na Ibrahim Bacca, kwani wenzao akiwamo Stephane Aziz KI, Diarra Djigui, Abuutwalib Mshery, Dickson Job, David Bryson, Denis Nkane na Shomary Kibwana wako na timu za taifa za Tanzania, Mali na Burkina Faso.

Baada ya mazoezi hayo Helmy, aliliambia Mwanaspoti kuwa kazi hiyo ingeendelea jioni kwenye uwanja wao wa mazoezi kule Avic Town, Kigamboni.

Helmy alisema: “Tulikuwa na mapumziko ya siku mbili tatu hivi ni lazima tuwe na mazoezi kama haya tunaporejea, lakini hii ni kuweka miili sawa kuelekea mechi zinazokuja, ratiba inayokuja ni ngumu lazima tuongeze utayari wa miili.”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad