Mwandishi wa Habari Zungu Fedha Afariki Kwa Kugongwa na Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa, mwandishi nguli wa habari na mdau wa masuala ya burudani, Shakoor Jongo maarufu kama ‘Zungu Fedha’ amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari usiku wa kuamkia leo, Septemba 4, 2022 katika maeneo ya Meridian Kinondoni jijini Dar.

Akizungumzia msiba huo, Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka amesimulia namna alivyoonana na Zungu usiku mpaka msiba ulivyotokea.

“Kulikuwa na shoo ya Twanga Pepeta huko Sinza, K-Garden karibu na kwa marehemu Banza Stone, mimi sikuingia ndani sababu nilikuwa natoka kwenye harusi ya CharlesBaba, nikiwa pale nikamuona Jongo akipita, nikamuita, ‘wewe Zungu njoo’ hakunisikia sababu ya muziki, alikuwa akipanda jukwaani kwa sababu muziki ulikuwa unapigwa.

“Baadaye mimi nikaondoka kwenda nyumbani. Nafika tu nyumbani naingia ndani ananipigia simu Kanoute mpiga solo wa Twanga, kwamba wametoka pale Twanga na Zungu, wamekuja sasa yeye Kanoute alikuwa ananunua chipsi, anaangalia anaona watu wapo katikati ya barabara.

“Kwenda kuchungulia anamuona Zungu lakini kagongwa na keshakufa na gari imekimbia. Ndipo akaomba wakampakia kwenye gari na kumpeleka hospitali ya Mwanayamala.

Zungu ambaye amewahi kuwa mwandishi wa Global Publishers kupitia magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikieenda, Risasi na Amani, alikuwa mdau mkubwa wa masuala ya Burudani.

Global Publishers inawapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa muziki kwa msiba huo.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitakuja baadaye.




-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad