Rais Willium Ruto Amkabidhi Uhuru Majukumu Mapya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Rais William Ruto amempa wajibu mpya mtangulizi wake, Rais wa mstaafu Uhuru Kenyatta kuwa msimamizi wa mipango ya amani ambayo Kenya imekuwa ikitekeleza katika eneo lote.


Katika hotuba yake ya kwanza kwa Taifa baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Nchi, Rais Ruto amedokeza kuwa Kenyatta amefanya kazi ya kupongezwa katika kusimamia mipango ya amani hasa nchini Ethiopia na Ukanda wa Maziwa Makuu.


Ruto ametangaza kwamba alikuwa amemwomba mtangulizi wake kuendelea na kazi hiyo, agizo ambalo yeye Rais Mstaafu Uhuru Kenyata alikubali.



Rais wa Kenya William Ruto akiwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta

“Kuhusu mipango ya amani katika ukanda wetu ikiwa ni pamoja na Ethiopia na Ukanda wa Maziwa Makuu, nimemuomba kaka yangu Rais Uhuru Kenyatta ambaye amefanya mashirikiano ya kupongezwa na mikoa hiyo na amekubali kuendelea kuongoza majadiliano hayo kwa niaba ya wananchi,” amesema Ruto.


Ruto apewa jukumu la kwanza Jumuiya Afrika Mashariki

Ruto amewahakikishia wakenya kuwa usimamizi wake utaunga mkono mipango ya amani ambayo itaongozwa na Kenyatta.


“Nimejitolea kuwa serikali ya Kenya na mimi mwenyewe haswa tutaunga mkono juhudi hizo ambazo zitaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. Na ninataka kuwashukuru kwa kukubali kwa moyo mkunjufu kutuunga mkono na kunisaidia katika afua hizo,” Ruto alisema.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad