Watu wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua MwanajeshiMahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro imewahukumu kunyongwa hadi kufa Watu watatu kwa kosa la kumuua Leonard Yamakwa ambaye alikuwa Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Akisoma hukumu hiyo yenye shauri namba 6 ya mwaka 2020 Msajili wa Mahakama ya Rufani Silivester Kahinda amewataja waliohukumiwa kuwa ni Charles, Hassan Athuman a Alfred Dotto ambapo amesema Washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo May 25, 2019 .


Amesema Washtakiwa hao siku ya tukio majira ya saa kumi na mbili za jioni walimkuta Leonard akiwa na Mpenzi wake katika mashamba ya Mikonge Tungi Manispaa ya Morogoro wakifanya mapenzi ndipo wakamtaka aondoke peke yake na aache pikipiki na Mwanamke jambo ambalo Leonard alikataa kutii

Baada ya Leonard kukataa Watuhumiwa walimshambulia na vitu vizito kichwani hadi kupoteza maisha kisha kumchukua Mwanamke huyo na kumbaka kila mmoja kwa wakati wake kisha waliondoka na pikipiki a simu za Leonard ambazo zilikuwa moja ya vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad