‘Lock down’ ya Ebola kwa Wilaya mbili, Wananchi walalama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Serikali nchini Uganda, imeweka vizuizi vya kusafiri katika wilaya mbili zilizokumbwa na virusi vya Ebola ikiwa ni njia mojawapo ya kukomesha kuenea kwa ugonjwa huo wa kuambukiza huku wakazi wa eneo wakidai kutengwa.


Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni alitangaza uamuzi huo utakaowafanya wakazi wa Wilaya za Kati za Uganda za Mubende na Kassanda kutoweza kusafiri ndani au nje ya maeneo hayo kwa njia binafsi au za umma.


Hata hivyo, magari ya mizigo na mengine yanayopita kutoka Kampala kuelekea kusini magharibi mwa Uganda yataendelea na kuruhusiwa kufanya usafirishaji.


Wadau wazindua uchunguzi udumavu wa Watoto


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Picha: Prime Business Africa

Siku ya Chakula Duniani: Vifo vya njaa jambo la kawaida

Maeneo yote ya burudani, ikiwa ni pamoja na baa, maeneo ya ibada yameamriwa kufungwa na mazishi ya mtu yeyote katika wilaya hizo sasa yanalazimika kusimamiwa na maafisa wa afya.


Museveni pia, ameweka amri ya kutotoka nje usiku, na hali hiyo itaendelea kwa takribani siku 21, huku Rais huyo akidai kuwa hatua hizo ni za muda zikilenga kudhibiti kuenea kwa Ebola.


Bilioni 2.2 wakabiliwa na uoni hafifu, upofu Duniani

Rais Samia afungua kituo cha umeme NyakanaziWadau wazindua uchunguzi udumavu wa Watoto

FacebookTwitterWhatsAppTelegramShare

You might also like


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad