Nairobi: Mwizi mmoja Auawa Katika Jaribio la Wizi wa Pesa Kwenye Benki ya Equity

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Walinzi wawili wamejeruhiwa baada ya kudungwa kwa kisu na wezi wawili waliokuwa na nia ya kuiba kwenye benki ya Equity huko Nairobi West.

Mwizi aliyewadunga kisu walinzi hao pia aliwajeruhi wateja wawili wa benki hiyo kwa kuwadunga kisu.


Mwizi huyo mmoja alipigwa riasi na maafisa wa polisi kisha kukata kamba papo hapo baada ya kujaribu kutoroka mandhari hayo.

Maafisa hao wa polisi walisema kuwa mwizi huyo alikuwa amejaribu kuiba pesa zilizokuwa zimeletwa kwenye benki hiyo na G4S huko Ghandi Avenue.

Kulingana na mashahidi, mwizi huyo mwengine alifanikiwa kutoroka baada ya kusababisha vurugu hiyo.


Barabara inayoelekea kwenye benki hiyo ya Equity imefungwa kwa muda ili kutuliza yaliyotendeka na kufanya uchunguzi wa wizi huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad