Kanisa la Pasta Ng'ang'a Lashuhudia Vitimbi Baada ya Waumini Kupigana Wakiondolewa Mapepo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Vioja na sarakasi zilishuhudiwa kwenye kanisa la Pasta Ng'ang'a baada ya waumini kuanza kupagawa kwenye madhabahu
Wengine wao walipigana mangumi na mateke huku baadhi ya wanaume wakionyeshana usogora wao wa karate wakati Ng'ang'a akikemea mapepo

Video iliyoonyesha matukio hayo ilizua mjadala mseto mitandaoni huku baadhi ya watu wakishangaa iwapo ni kweli au waumini walikuwa wakijidai

Video iliyomnasa Pasta James Ng'ang'a akiyaondoa mapepo kutoka kwa waumini wake, imewasha mitandao ya kijamii huku wengi wakishangaa iwapo ni kweli au walikuwa wakiigiza.

Kanisa la Pasta Ng'ang'a Lashuhudia Vitimbi Baada ya Waumini Kupigana Wakiondolewa Mapepo
Pasta Ng'ang'a akikemea mapepo wakati wa ibada ya kanisa. Picha: Channel 7.

Kwenye video fupi iliyosambazwa na katika Facebook na Channel 7 News, wanawake walianza kuanguka kwenye madhabahu baada ya Ng'ang'a kukemea kwa jina la Yesu Kristo.

TUKO.co.ke haijabainisha ni nini kilichokuwa kikiendelea ila kwa kukagua video hiyo, pasta huyo alionekana kuoyaondoa mapepo.

Waumini hao, wengi wakiwa ni wanawake walianza kufoka na kupagawa kwenye madhabahu, huku Ng'ang'a akiwashabikia.



Baadhi ya wanaume walijiunga kwenye sarakasi hizo na kuanza kupiga miereka, na kuzidi kfanya wengi kuchanganyikiwa hata inagwa hawakuumuzana.

Matukio hayo yalionekana ni kama mchezo wa kuigiza, na dakika za mwisho Ng'ang'a aliwaambia walisifu jina la Yesu Kristo.


Wakenya watoa maoni kuhusu video hiyo.

Mohamed Hussein Saadad:

"Nijuavyo, ukiamini umepona basi umepona tayari. Haihusiana kivyovyote na miujiza au pasta Nganga."


Mboya Denis:

"Sasa vitimbi vya nini? Ninachoona na mchezo wa kuigiza huku kukiwa na waigizaji waliopewa mafunzo. Hongera pasta nganga."

Edson Bukenya:

"Afrika imejaa vitimbi, ni Mungu aingilie kati!"

James Lukindo:

"Hiyo ni drama ya miujiza kwenye makanisa pekee. Ikiwa ni kweli wanaponya na kukemea mapepo kwa nini wasiendee hospitalini ambako watu wengi wanateseka?"
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad