Padri Soka Anayekabiliwa na Tuhuma za Kubaka Apata Pigo Jipya kanisani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Moshi. Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, limemuamuru Padri Sosthenes Bahati Soka (41) anayekabiliwa na mashtaka ya kubaka watoto watatu wa kike kuondoka katika nyumba za kanisa hilo.

Badala yake, barua ya Askofu wa Jimbo hilo, Ludovick Minde ya Septemba 26, mwaka huu ambayo gazeti hili limeona, amemweleza Padri huyo haruhusiwi kuishi katika nyumba za kanisa na atakuwa akiishi nyumbani kwa wazazi wake.

Hili linaweza kuwa pigo jingine kwa Padri huyo ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kesi zake, baada ya kanisa pia kumsimamisha kutoa huduma zote za kipadri katika kanisa hilo kubwa duniani.

Katika barua yake hiyo ambayo imesambaa mitandaoni, Askofu Minde alisema uamuzi huo umezingatia sheria ya kanisa namba 1,722 inayotaka mtuhumiwa kutengwa katika kipindi cha mchakato wa kisheria wa tuhuma zinazomkabili.


Sheria hiyo inasema ili kuzuia kashfa, kulinda uhuru wa mashahidi na kulinda njia ya haki, watu wa kawaida, baada ya kumsikiliza mtetezi wa haki na kumtaja mtuhumiwa, katika hatua yoyote ya mchakato inaweza kuwatenga mtuhumiwa na kazi za kikanisa.

Pia, sheria hiyo inasema kanisa linaweza kuweka au kumkataza kuishi mahali fulani au eneo fulani au hata inaweza kukataza ushiriki wa umma katika Ekaristi Takatifu zaidi na mara tu tuhuma zinapokoma na hatua hizi zote lazima zifutwe na pia huisha na sheria yenyewe pale mchakato wa adhabu unapokoma. “Kwa masikitiko makubwa, kwa barua hii kuanzia leo tarehe 26/09/2022 umesimamishwa kutoa huduma zote za kipadri katika Kanisa Katoliki, pia huruhusiwi kuishi katika nyumba za kanisa. Utakuwa unaishi nyumbani kwa wazazi wako,” alisisitiza Askofu Minde katika barua hiyo na kuongeza:

“Lengo hasa la maamuzi haya ya awali ni kupisha vyombo vya sheria, ili uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma husika ufanyike na mahakama zote husika.


“Iwapo vyombo vya sheria vitatuhakikishia kwamba hukuhusika kwa namna yoyote katika mashtaka yanayokukabili, basi kanisa litakuwa tayari kukupokea tena, na pia kukuruhusu kuendelea kutoa huduma za kipadri”.

Nakala ya barua hiyo imetumwa kwa mapadri wote wanaotoa huduma katika jimbo Katoliki la Moshi, wakiwemo walioko katika taasisi ambao kwa mujibu wa tovuti ya Kanisa Katoliki jimbo la Moshi ya www.moshidiocese.org ni zaidi ya 130.

Juzi, Katibu Mkuu wa Baraza la Maasofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima alinukuliwa na gazeti hili akisema tayari Askofu Minde alikuwa amemsimamisha Padri huyo kufanya kazi.

“Kwa sasa Askofu amemsimamisha kutoa huduma za kipadri mpaka mahakama ifanye maamuzi yake. Baada ya hapo ndipo maamuzi mengine juu ya upadri yatafanyika,” alisema Padri Kitima, kauli inayofanana na ya barua ya Askofu Minde.


Mashtaka yanayomkabili

Katika kesi ya kwanza alidaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12, Agosti 12, 2022 katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mt. Dionis Aropagita iliyopo barabara ya Kawawa katika Wilaya ya Moshi.

Mshtakiwa alikana tuhuma na upande wa mashtaka ukaiarifu mahakama upelelezi wake umekamilika na mahakama ikapanga Oktoba 10, upande wa mashtaka utamsomea maelezo ya kosa.

Mshtakiwa alipewa dhamana yenye masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaojaza hati ya dhamana (bond) ya Sh10 milioni, alitimiza masharti.

Katika shtaka lingine alidaiwa kumbaka mtoto wa umri wa miaka 13 katika eneo hilo hilo la Parokia.


Mahakama ilisema dhamana iko wazi na kumtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya Sh2.5 milioni na atasomewa maelezo ya awali Oktoba 12.

Katika kesi ya tatu ilidaiwa mshtakiwa alimbaka mtoto wa miaka 12 katika eneo hilo hilo la Parokia.

Alikanusha mashtaka na mahakama ilimpa dhamana yenye masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya Sh2 milioni. Upelelezi wa kesi umekamilika na atasomewa maelezo ya awali Oktoba 18.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad