Christian Ronaldo "Wayne Rooney Ananionea Wivu Sababu Nimemzidi Kila Kitu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Sehemu nyingine ya mahojiano ya mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo na Piers Morgan, amemjibu mshambulaji wa zamani wa Klabu hiyo, Muingereza Wayne Rooney ambaye aliwahi kumkosoa siku za hivi karibuni.

"Sijui kwanini Wayne Rooney ananikosoa sana, pengine kwakuwa bado nacheza muda mrefu tena kwenye ushindani mkubwa kuliko yeye, hilo sifahamu." - ameeleza Ronaldo na kuendelea.

"Ananionea wivu kuona naendelea kucheza mpira hadi leo na tulianza pamoja, sio hivyo tu hata muonekano nimemzidi kwa sasa." - Ronaldo.

Itakumbukwa, Rooney kwenye mahojiano yake na Gazeti la Times, mwezi Agosti mwaka huu alisema angekua kocha wa Man United, asingekuwa anampanga Ronaldo kwani bado akili yake haipo sawa kabisa kwa upande wake, akisisitiza mwamba bado hayupo fiti asimilia 100.

“Nisingemchezesha Ronaldo na Marcus Rashford, endapo ningekua upande wa Ten Hag hawa wawili nisingewapanga kabisa, Man United haina budi kumtegemea Ronaldo lakini sioni kama yupo fiti, anaonekana anahitaji muda zaidi wa kurudi katika kiwango chake,” - alisema Rooney kwenye mahojiano na Gazeti la Times, Agosti mwaka huu.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad