Mwanaume Mmoja Akutwa Amefariki Katika Bwawa Dogo Mjini Njombe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 amekutwa kafariki ndani ya Bwawa dogo mjini Njombe
MWANAUME mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 mpaka 35 amekutwa amefariki katika Bwawa dogo lililopo katika Msitu wa TANWAT eneo la Kibena Mjini Njombe.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni Walinzi katika Msitu ya Tanwat uliopo karibu na Bwawa hilo wamesema kuwa mnamo majira ya saa 11;10 Alfajiri ya tarehe 21 hi leo waligundua uwepo wa mtu ambaye alikuwa kisogea katika Bwawa hilo huku akiwa ameshika Tochi na baada ya Kufika akaanza kuingia ndani ya Bwawa hilo na hata walipojaribu kumuita ili atoke nje ya Bwawa Hakuwasikiliza.

 

Akizungumza na Vyombo vya Habari baada ya kuutoa mwili katika Bwawa Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Njombe, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Inspekta Joel Mwakanyasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Baada ya Mwili Huo kutolewa katika Bwawa, Jeshi la Zimamoto liliwataka wananchi kuutambua mwili huo lakini Wananchi akiwemo George Mlangwa wamekiri kutomfahamu mtu huyo.

 

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Njombe limewaasa Wananchi kuacha mara Moja tabia ya kusogelea maji yenye kina kirefu ikiwa hawana Uwezo wa kuogelea.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad