Nape azungumzia kupanda bei bando

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hakutakuwa na mabadiliko ya bei za bando yoyote hadi tathmini ya gharama itakapokamilika.

Tathmini hiyo inayofanywa kila baada ya miaka mitano, inatarajiwa kukamilika kati ya Desemba 2022 hadi Januari 2023.

Ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 21, 2022 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.

Nape amesema kwa sasa watoa huduma wote wako katika viwango vya bei elekezi iliyowekwa na Serikali ambayo ni kati ya Sh2.03 hadi Sh9.35.


"Hatutegemei mabadiliko yoyote kwa kipindi hiki hadi tathmini itakapokamilika, niwaombe wananchi wasione hatuhangaiki na suala hili, tumekuwa tukihangaika nalo."

"Sasa tumefikia hatua ambayo tumesema tutatulia hadi tathmini itakapokamilika na matumaini yetu kuwa itatupa muelekeo mzuri," amesema Nnauye

Hiyo ni kutokana na kile alichokieleza tathmini itaelezea uwekezaji uliofanyika, hatua za kikodi zilizochukuliwa, marekebisho yaliyofanyika na itatoa matokeo kuwa gharama zinaweza kushuka kwa kiasi gani.


"Lakini wakati tukisubiri matokeo ya tathmini hiyo hakutakuwa na mabadiliko na tumewataka TCRA kwani wanapaswa kupelekewa maombi ya mabadiliko kuwa kwa sasa watulize sekta watu waendelee kutumia huduma," amesema

Hili linafanyika ikiwa ni muendelezo wa ushughulikiaji malalamiko ya wananchi juu ya upandaji holela wa vifurushi unaofanywa na mitandao ya simu jambo ambalo limekuwa likifanya vilio kusikika kila kona.

Malalamiko hayo yamekuwa yakijikita zaidi katika bando la intaneti, kwa mfano mtandao mmoja nchini umebadilisha bei za kifurushi cha data kilichouzwa kwa Sh1,000 awali kiliwezesha megabaiti 450 kwa wiki, lakini sasa kwa bei hiyo zinapatikana megabaiti 350 sawa na upungufu wa asilimia 10.

Pia, kifurushi cha Sh 20,000 kilichokuwa kikitoa gigabaiti 12 kwa siku 30 hivi sasa kinatoa gigabaiti 9.5 kwa siku 30. Sh2, 000 iliyokuwa ikinunua gigabaiti 1.1 kwa siku tatu hivi sasa inanunua megabaiti 985.
Robati Gwaki
5h
2

nyie wezi tu hamna lolote Tena wewe Waziri inatakiwa ujiuzuru maana wewe mda wote hutetei raia uko upande wa hayo makampuni tu
Jibu
majibu 3


GUEST_oMyz2Jzzb
2h

nape mwenyew mwizii wa nchii hii atumuelew wanatupeleka jinsi wanavyo taka Ila Mungu anawaona ipo siku Mungu atatutoa kwenye hiki kizazi kisicho na uruma na wananchii wakee haiwezekaniki mm nanunua bando langu nisipo litumia wanalichukuwa niulize tu wanalichukuwa wanalipeka wapiii iviii ata mm ambaye sijasoma naona hili Ni tatizo yeye Nape ahoni Kam Ni tatizo kwelii inawezekan????? nape na januri makamba tumewakabidhi mikononi mwa MunguZaidi


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad