Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa wakati wa Utaji Saini wa Mkataba wa Ujenzi wa kipande kingine cha Reli ya SGR LOT 6 kati ya Tabora hadi Kigoma
Kadogosa amesema "Tumenunua Mabehewa 59, ambapo Mabehewa 14 mapya tayari yameingia Nchini. Kuna Mabehewa 30 na Vichwa Viwili 'Used' vitaingia kati ya Machi na Aprili 2023
Ameongeza kuwa kulikuwa na matatizo na Msambazaji wa kwanza kutoka Uturuki na Shirika lilivunja Mkataba naye baada ya kushauriana Serikalini na kumpa Msambazaji mwingine wa Ujerumani kwa ajili ya kumalizia kazi.