Aliyebaka na Kuua Mke wa Mwenyekiti Amakatwa..Njaa Yamtoa Mafichoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumkamata kijana Paschal Kaigwa (22) mzaliwa wa Kishogo Bukoba Vijijini, ambaye anatuhumiwa kumbaka na kumuua mke wa mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata ya Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba, aitwaye Khadija Ismail (29)



Kamanda wa polisi mkoani Kagera William Mwampaghale amesema kuwa mtuhumiwa huyo alijificha katika vichaka na kwamba baada ya kukaa huko bila chakula, aliamua kutoka mafichoni na kwenda nyumbani kwa shangazi yake katika mtaa wa Katatorwansi ulioko katika manispaa ya Bukoba


Imeelezwa kuwa alipofika alikuta watoto ambao baada ya kumuona walipiga kelele na kuwezesha wananchi kumkamata.


"Njaa ilimtoa mafichoni akaenda kwa shangazi yake, lakini watoto aliowakuta pale walikuwa tayari wana taarifa, kutokana na taarifa zenu mlizozitangaza kuwa anatafutwa, tumemkamata juzi tarehe 19/02/2023 saa kumi jioni, tunaye tunamhoji na tutamfikisha kwenye vyombo vya kishera" amesema Kamanda Mwampaghale


Februari 13 mwaka huu majira ya jioni, kijana huyo ambaye alikuwa amepewa hifadhi nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa huo kutokana na kutokuwa na mahali pa kuishi, anadaiwa kumbaka na kumuua mke wa mwenyekiti na kisha kutoweka

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad