Nabi Ashtukia Jambo Zito Young Africans

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddin Nabi amesisitiza jambo zito kwenye kikosi chake, kuelekea mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, dhidi ya AS Real Bamako.


Young Africans itacheza ugenini mjini Bamako keshokutwa Jumapili (Februari 26), ikiwa na morari ya hali ya juu baada ya kuibamiza 3-1 TP Mazembe, kwenye mchezo wa Mzunguuko wapili uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa mwishoni mwa juma lililopita.


Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesisitiza kutoa nafasi kwa wachezaji wenye umihimu na wanaojituma mazoezini katika kikosi chake cha kwanza, ambacho kitakuwa na jukumu la kusaka alama tatu dhidi ya AS Real Bamako.


Onyango ashusha PRESHA Simba SC

Nabi amesema kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika kikosi chake cha kwanza, lakini bado kuna baadhi yao wamekuwa wanahisi kama wameshafanikiwa, jambo ambalo analipinga vita kila kukicha.


“Kila mchezaji anatakiwa kupata nafasi ndiyo maana ya timu, niliona kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi kulingana na ratiba tuliyonayo mbele yetu, lakini nimesikitishwa na viwango vya baadhi ya wachezaji ambao hawaonekani kubadilika,”


Robertinho: Tunazihitaji alama tatu Uganda

“Kuna wachezaji ambao wameridhika, hawaonyeshi kuwa na shauku ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, hiyo ni mbaya na ni kitu ambacho hakitakiwi kuwa kwenye klabu kama hii yenye malengo makubwa.” amesema Nabi


Tayari kikosi cha Young Africans kimeshawasili mjini Bamako tangu jana Alhamis (Februari 23), na leo kimeanza mazoezi mjini humo kuelekea mchezo wa Jumapili.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad