Ticker

6/recent/ticker-posts

Mchambuzi Shaffi Dauda Aingilia kati Sakata la Feitoto kuitwa Timu ya Taifa, Ahoji Hawa Waliokosekana

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


 KAPOMBE, ZIMBWE Jr, WAMESTAAFU?

Kwa upande wangu sijashangaa Feitoto kuitwa Taifa Stars ila ningeshangaa kama asingeitwa. Nilichoshangaa ni kutomuona Shomari Kapombe na Mohamed Hussein!


Au Kapombe na Mohamed Hussein wamestaafu? Kwa sababu wito wa timu ya Taifa wachezaji hawasubiri kusikia kupitia vyombo vya habari. Kwa kawaida huwa kuna taarifa rasmi ambayo inatumwa na Shirikisho kwenda kwa klabu kwamba mchezaji fulani ameitwa kujiunga na timu ya Taifa anapaswa kuripoti kambini siku fulani.


Baada ya hapo klabu inampa taarifa mchezaji. Sasa mchezaji anaweza kusema kwa kipindi husika anatamani kuweka nguvu zake kwenye klabu yake kwa hiyo anaijulisha klabu ilijibu Shirikisho halafu na yeye anaandika barua kwa Shirikisho kulitaarifu kwa kipindi husika jina lake lisijumuishwe lakini atakuwa tayari kwa wakati mwingine.


Kwa mantiki hiyo, hauwezi kulaumu kwa nini mchezaji fulani hajajumuishwa kwenye kikosi cha Taifa. Ni muhimu kufatilia kujua kwa nini mchezaji hajaitwa ili kupata taarifa.


Kwa hiyo nilitamani kusikia kutoka kwa Kocha kwa nini hawajawaita Shomar na Mohamed Hussein ambao kwa sasa wapo kwenye ubora wao na ni senior kwenye kikosi cha Stars.

Post a Comment

0 Comments