Nahodha Horoya AC: Tutaishangaza Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPANahodha wa Mabingwa wa Soka nchini Guinea Horoya AC Ocansey Mandela amesema jambo lililowaleta Tanzania ni moja tu, kushinda mchezo dhidi Simba SC, ili wajisafishie njia ya kutinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, msimu huu 2022/23.

Horoya AC itakua mgeni wa Simba SC leo Jumamosi (Machi 18) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ukiwa mchezo muhimu kwa pande zote mbili, ambazo zinahitaji ushindi.

Mandela amesema anaamini maandalizi yao kuelekea mchezo wa leo yanatosha kuishangaza Simba SC, kama ilivyowahi kushangazwa katika baadhi michezo ya Kimataifa kwenye wao wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Hatuwezi kutoka Guinea kuja kupoteza, tumekuja kushinda ili tujisafishie njia ya kwenda Robo Fainali, na kama ambavyo timu zingine zimepata matokeo hapa basi hata sisi tutapata matokeo pia mashabiki wao wajiandae kisaikolojolia”

“Tupo kwenye Michuano hii kwa ajili ya kupambana, tumejiandaa vizuri kuikabili Simba SC ambayo tunaiheshimu sana kwa sababu ipo nyumbani kwao, tunajiamini kwa kuwa tumejiandaa kushinda hapa Dar es salaam.” Amesema Mandela

Endapo Simba SC itashinda leo Jumamosi (Machi 18) dhidi ya Horoya AC itafikisha alama 09 na kutinga moja kwa moja Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na kuungana na Raja Casablanca ya Morocco iliyojikusanyia alama 12 hadi sasa.

Na ikitokea Horoya AC inaibuka na ushindi dhidi ya Simba SC, Miamba hiyo ya Guinea itafikisha alama 07, ambazo zitaifanya kusubiri hadi katika mchezo wa mwisho wa Kundi C utakawakutanisha dhidi ya Vipers SC ya Uganda nyumbani kwao, ili kujua hatma yao.
________________

KISASI CHA USALITI PENZINI !!!,usipoipenda simulizi hii dai Mb na pesa zako,licha ya kuenjoy mahaba ndani yake kuna kitu cha kujifunza mwishoni Bofya Hapa kusoma Sehem ya 1 bure,sehem iliyobaki tsh 2000 kwa mtandao wowote.

Tembelea www.makapedia.com kwa stori mpya kila tarehe moja.


JE UNATAKA BIASHARA YAKO IWE YA UHAKIKA MIAKA YOTE YAJUE HAYA? usikose kitabu hiki Bofya Hapa kusoma sehem ya 1 bure sehem ya 2 tsh 2000 tu 

ndani ya www.makapedia.com

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad