Watu 9 Wafariki Ajalini, 30 Wajeruhiwa Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi – Video

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Watu 9 akiwemo Mama mjamzito wamefariki Dunia na wengine 30 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka na kudondokea bondeni katika mlima wa Nkondwe wilayani Tanganyika mkoani Katavi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema ajali hiyo ilitokea Alasiri ya Machi 6, 2023 ikihusisha basi kampuni ya Komba’s. Amebainisha kuwa baada ya kufika katika mlima huo gari liliserereka na kudondokea kwenye bonde kubwa lenye kina cha mita zisizopungua 75.


“Chanzo cha ajali hakijajulikana na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea na uchunguzi huku zoezi la kuitambua miili likiendela kwa ajili ya taratibu zingine,” amesema.


Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Dk. Alex Mrema amethibitisha vifo hivyo vimetokea papo hapo ambapo kati ya waliofariki wanaume ni wawili, watoto 3, wanawake wanne akiwemo mjamzito.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad