Yanga yapanda katika viwango vya ubora CAF yashika nafasi hii
 Baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamepanda katika viwango vya ubora CAF

Yanga imepanda mpaka nafasi ya 27 kutoka nafasi ya 75 waliyokuwa msimu uliopita

Yanga imekusanya alama 10 katika michuano ya Shirikisho msimu huu

Wananchi wana nafasi zaidi ya kupanda kama watafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali kwenda nusu fainali, kuingia fainali na hata kutwaa ubingwa

Aidha Tanzania imepanda mpaka nafasi ya saba katika viwango vya ubora baada ya klabu za Simba na Yanga kutinga robo fainali ya michuano ya CAF
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad