Haji Manara Ampigia Magoti Benard Morison na Kusema Haya 'Miguu yako ni Dhahabu Waburuze Waarabu Kwenye Box''

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Benard Morrison na Haji Manara
Benard Morrison na Haji Manara

Ameandika Haya Haji Manara: 

"Bernard Bernard Bernard Bernard Bernard Bernard,unaona nimekuita mara ngapi rafiki yangu? Unajua mimi naamini katika wewe? Unakumbuka maneno niliyokwambia Havock usiku kipindi unarudi Yanga?

Kuna Wanayanga wachache hawakutaka urudi baada ya kuwaacha, nikafanya Press maalum kuelezea umuhimu wako,huku nikijitolea mfano hai mimi mwenyewe, nikiwakumbusha kama mlinipokea mimi nileyekuwa Kolo mkorofi, shida nini kwa Morrison?

Nivishe nguo,Na Msitiri Rais wetu Hersi @caamil_88 , Tupe ulichonacho Wananchi, Miguu yako ni dhahabu bro, unaweza kuamua mechi hizi , wewe kwangu ni kipaji kikuu, Your only player kwenye ligi yetu unaeweza kuteketeza mabeki Kwa chenga za kuwafuata, unajua unajua unajua hadi unakera.

Anza kumuonyesha Kocha kwamba unaitaka hii mechi mazoezini, weka focus yako yote kwenye fainali ya hizi game mbili, tunaiamini miguu yako Mwamba , kawachezesha ngoma ya kwenu Waarabu, kapige yale Madegejee yako yenye faida kwa Team, kawaburuze Waarabu kuwaleta kwenye box....

Ahhh Ben my brother, nitakupa kidani cha dhahabu ukifanya nitakayo ili umpelekee Mama yetu Ghana.

Nnavyokujua ukicheza kwa spirit ya Team hakika ndoo ya Afrika tunaipokea Dar tarehe nne June, amua kuhusu hii mechi, au hutaki mpunga mwingi? NAKUAMINIA MY BEST FRIEND." Manara

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad