India Yatoa Msamaha wa Faini Kwa Watanzania Waliokwama Kurudi Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Msamaha unawahusu waliopitisha muda wao wa ukaazi Nchini #India na kushindwa kulipa faini ya ‘Exit Permit’, ambapo msamaha ni kuanzia Mei 2023 hadi Oktoba 31, 2023

Balozi wa #Tanzania Nchini India, Anisa Mbega amesema “Kuna Watanzania wengi walioshindwa kulipa kutokana na kutokuwa na Fedha lakini baada ya mazungumzo kati yetu na Mamlaka za India hatimaye Watanzania watanufaika.”

Ameongeza "Watanzania wanaokabiliwa na kesi mbalimbali hawatahusika hadi hapo utaratibu wao wa kisheria utakapoamilika."

Pia ametoa wito “Watakaofanikiwa kurejea Nyumbani hasa dada zetu mkawe Mabalozi wazuri, mkawaeleze wenye Ndoto za kuja India kwa njia ambazo mlipitia ninyi, changamoto mlizokutana nazo ili wasije wakaingia katika madhira ambayo mmekumbana nayo.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad