Mwamba Aliyehukumiwa Kimakosa Aachiliwa huru Jela Baada ya Miaka 33

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwamba Aliyehukumiwa Kimakosa Aachiliwa huru Jela Baada ya Miaka 33


Mwanasheria Mkuu wa wilaya ya Kaunti ya Los Angeles George Gascón ametangaza kuwa Daniel Saldana, ambaye sasa ana umri wa miaka 55, ameachiliwa huru baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 45 jela mnamo mwaka 1990 kwa kosa la kufyatulia risasi gari iliyokuwa ikitoka kwenye mchezo wa soka wa skuli moja ya sekondari iliyoko kwenye bustani ya Baldwin, mashariki mwa Los Angeles.


Ufyatuaji risasi huo ulipelekea kujeruhiwa vijana wawili kati ya sita waliokuwamo ndani ya gari hilo lakini hawakufariki.


Saldana alikuwa mmoja wa wanaume watatu walioshtakiwa kuhusika na shambulio hilo na akahukumiwa kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa sita ya kujaribu kuua na shtaka moja la kufyatulia risasi gari lililokuwa na watu ndani yake.


Erdogan asifu ushindi wake kama ushindi wa demokrasia


Tinubu kuapishwa rasmi leo, Rais Samia awasili kushuhudia

Hata hivyo ushahidi uliotolewa na mshambuliaji mwingine wa tukio hilo aliyehukumiwa ulibainisha baadaye kwamba Saldana “hakuhusika kwa namna yoyote ile katika ufyatuaji risasi na wala hakuwepo wakati wa tukio hilo.”


Mwanasheria Mkuu wa wilaya ya Kaunti ya Los Angeles amemuomba msamaha Saldana na familia yake, akisema, “ninajua kwamba hii haitakurudisha nyuma ya miongo uliyosota gerezani, lakini natumai kuomba kwetu radhi kutakupa faraja japo kidogo wakati unaanza maisha yako mapya”.


Raia wahamasishwa kubeba silaha, kupambana

Gascón ameongezea kwa kusema: “sio tu hili ni janga la kuwalazimisha watu kufungwa gerezani kwa uhalifu ambao hawakufanya, lakini kila pale haki inapokosa kutendeka kwa ukubwa kama huu, wahusika halisi huwa wangali wako nje wakifanya uhalifu mwingine”.


Kufikia Februari 2020, jumla ya watu 2,551 waliofutiwa mashtaka baada ya kuhukumiwa na kufungwa jela walitajwa katika Masijala ya Taifa ya Waliosamehewa nchini Marekani. Muda wote ambao watu hao walioachiliwa huru walisota magerezani unafika miaka 22,540

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad