Mrithi Wa Joash Onyango Kimeeleweka Simba Ahmed Ally Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mrithi Wa Joash Onyango Kimeeleweka Simba Ahmed Ally Afunguka

TAARIFA zinasema kuwa Simba imeanza mazungumzo rasmi na Klabu ya Cotton Sports ya Cameroon kwa ajili ya kumsajili beki wa kati wa timu hiyo, Che Fondoh Malone ambaye anatajwa kuwa mrithi wa beki, Joash Onyango ambaye amewasilisha barua ya kutaka kuondoka kikosini hapo.


Hiyo ni katika kuelekea usajili wadirisha kubwa litakalofunguliwa hivi karibuni wakati Ligi Kuu Bara imemalizika. Simba tayari imeanza kufanya usajili wa kikosi chake, ikiwa imemsajili tayari mshambuliaji wa Rayon Sports ya Rwanda, Willy Onana.


Taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, tayari mazungumzo kati ya uongozi wa Simba na wasimamizi wa mchezaji huyo, Royal Soccer Management yameanza kwa ajili ya kumsajili.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa upo uwezekano wa beki huyo kujiunga na Simba kutokana na menejimenti ya mchezaji huyo kugomea baadhi ya ofa kadhaa ambazo wamepelekewa mezani.


Aliongeza kuwa kama mazungumzo yakienda vizuri, basi beki huyo atatua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la mkataba wa miaka miwili.


“Katika dirisha la usajili la mwezi Januari baadhi ya klabu zilionyesha nia ya kumuhitaji Malone, lakini yeye mwenyewe amegomea na kusimamia msimamo ya kuja kuichezea Simba.


“Hivi sasa mazungumzo yanakwenda vizuri, hivyo muda wowote atatua nchini kwa ajili ya kukamilisha dili la usajili katika kuelekea dirisha kubwa la usajili,” alisema mtoa taarifa huyo.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu wa Simba, Ahmed Ally akizungumzia masuala ya usajili ya timu hiyo, alisema: “Mazungumzo yanakwenda vizuri na baadhi ya wachezaji, mara baada ya usajili huo kukamilika kila kitu tutaweka wazi.”


STORI NA WILBERT MOLANDI

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad