Viingilio Yanga Vs Asas Fc CAF Confederation Cup Leo Tarehe 26 August 2023

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Viingilio Yanga Vs Asas Fc CAF Confederation Cup Leo Tarehe 26 August 2023



 Viingilio Yanga Vs Asas Fc CAF Confederation cup leo Tarehe 26 August 2023

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex siku ya Jumamosi, August 26 katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Asas Fc

Kamwe amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujihakikishia tiketi ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ikiwa ni hatua moja kuelekea makundi

"Mchezo huu haujamalizika kama wengi wanavyosema. Unapodharau mpinzani kwa sekunde moja tu, mechi inaweza kubadilika. Iko mifano mingi tu, kuna timu ziliwahi kushinda ugenini na kupoteza nyumbani"

"Kwa kuwa tuna dakika 90 za kucheza hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu. Tunaomba mashabiki wetu mje kwa wingi kushangilia ili kuhakikisha tunasonga mbele. Nawaomba mashabiki tusiingie katika mtego wa kudhani mechi imemalizika"

Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo ambapo Mzunguuko ni Tsh 5,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na VIP A ni Tsh 30,000/-

Kamwe amewaasa mashabiki kuhakikisha wananunua tiketi zao mapema, wasisubiri kukata tiketi uwanjani kwani kuna matukio ya kuuziwa tiketi feki

Aidha Kamwe amesema siku hiyo imepewa jina la 'Max Day', Wananchi wataitumia kumuenzi mchezaji wao Max Nzengeli kwa kuchomekea

"Kwa yeyote atakayekuja uwanjani ahakikishe amechomekea, huu ndio utakuwa mtoko wetu wa Max Day,"

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad