Straika Wa Mabao Hana Furaha Simba, Mashabiki Wapata Mchecheto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Straika Wa Mabao Hana Furaha Simba, Mashabiki Wapata Mchecheto

 Straika Wa Mabao Hana Furaha Simba, Mashabiki Wapata Mchecheto

Mshambuliaji wao raia wa Zambia, Moses Phiri

HABARI mbaya kwa mashabiki wa Simba zinadai kuwa mshambuliaji wao raia wa Zambia, Moses Phiri hana furaha ndani ya timu hiyo na huenda akaondoka kikosini hapo kama mambo yataendelea kuwa magumu kwake.


Phiri ndani ya Simba amekuwa na wakati mgumu kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Msimu uliopita Phiri alianza ligi kuu kwa kasi alifunga mabao 10 na baada ya hapo akakumbwa na majeraha yaliyomfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.


Simba chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Robertinho limekuwa likiwatumia zaidi washambuliaji John Bocco sambamba na Jean Baleke tofuati na Phiri ambaye amekuwa akisugua benchi mara kwa mara.


Chanzo chetu makini kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Ijumaa juu ya mshambuliaji huyo kutokuwa na furaha na kuwekwa benchi mara kwa mara na inadaiwa kwa sasa Mzambia huyo ana mipango ya kuondoka ndani ya timu hiyo endapo ataendelea kusugua benchi.


“Phiri hana furaha kabisa kwa sasa ndani ya simba kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, na tayari anafikiria kuondoka kama hali itaendelea kuwa hivi ilivyo.


“Malengo makubwa ya Phiri yalikuwa ni kuisaidia Simba katika michuano ya ndani ya kimataifa lakini kote huko amekosa kipaumbele, baada ya kupona alitarajia kuwa angepata nafasi lakini hilo limeshindikana,” kilisema chanzo hicho.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad