Ujenzi BRT Mwendo Kasi Posta Hadi Boko Kuanza wiki ijayo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


 Ujenzi BRT Mwendo Kasi Posta Hadi Boko Kuanza wiki ijayo

Wakati Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (Dart), ukianza ujenzi wa kutanua kituo chake cha Kivukoni, ujenzi wa miundombinu ya kupita mabasi hayo kwa barabara ya Bibi Titi, Ali Hassan Mwinyi na Sam Nujoma utaanza Oktoba 15, mwaka huu.


Hayo yalisemwa jana na Kaimu Meneja wa Mipango ya Usafirishaji wa Dart, Mhandisi Mohammed Kuganda alipokuwa akizungumzia ujenzi mbele ya waandishi wa habari.


Kuganda alisema ujenzi huo ni wa mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) awamu ya nne ukitanguliwa na ule wa barabara ya Morogoro (awamu ya kwanza), barabara ya Mbagala (awamu ya pili) na awamu ya tatu ikihusisha barabara ya Nyerere.


Meneja huyo alifafanua zaidi kuwa ujenzi huo utaanzia maeneo ya Maktaba Kuu Barabara ya Bibi Titi kupitia Mwenge na kisha Mawasiliano ambayo itaenda kukutana na daraja la Ubungo.


Alisema ujenzi mwingine utaanzia Mwenge kwenda Boko Dawasa.


Alisema barabara zote hizo zinatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh400 bilioni zikiwa na urefu wa kilometa 30.1 na kila barabara itakuwa na mkandarasi wake.


Kituo cha Kivukoni


Akizungumzia kituo cha Kivukoni, Kuganda alisema ujenzi utaanza Oktoba 21, baada ya kituo cha daladala kuhamishwa.


"Kukamilika kwa awamu hizi za ujenzi wa barabara pamoja na awamu ya tano na ya sita, utakifanya kituo che Kivukoni tunachoenda kukitanua kuhudumia zaidi ya mabasi yetu 3,200, hivyo utaona namna gani kunahitajika eneo kubwa na la kutosha kuingia mabasi hayo," alisema Kuganda.


Akielezea utaratibu wa kuondolewa kwa kwa kituo cha daladala, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Dart, Willium Gatambi, alisema utazihusisha daladala zilizokuwa zikifanya safari zake maeneo mbalimbali na kuishia kituo hicho , ambapo mwisho wa kutumia eneo hilo ni Oktoba 20.


“Kuisha kwa ujenzi wa awamu hizi ni wazi kuwa kutakuwa na ongezeko la mabasi na hivyo kutulazimu kutanua zaidi kutuo chetu kuliko ilivyo sasa, ndio maana yanaanza maandalizi mapema,” alisema Gatambi.


Alitaja vituo ambavyo daladala hizo zitaishia kuwa ni pembezoni mwa ukuta wa Wizara ya Ardhi ikihusisha magari yanayotoka Kigogo Sokoni, Tabata Chang'ombe,Tabata Kinyerezi, Buyuni Sokoni na Machinga Complex.


Kituo kingine ni NBC maarufu Posta ya zamani. Alisema kituo hicho kitahusisha daladala zinazotoka Kisemvule, Kivule Sokoni na Mbande Kisewe.


Wakati kituo cha tatu kitakuwa ni Mtaa wa Ohio kikihusisha daladala zinazotoka Gonglamboto na Tegeta Nyuki.


"Hata hivyo, mabadiliko hayo hayatazigusa bajaji kwani zenyewe zitakuwa zikiegesha pembezoni mwa uzio utakaowekwa wakati ujenzi ukiendelea," alisema Gatambi.


Katibu wa Umoja wa wamiliki wa daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Shifwaya Lema akizungumzia ujenzi huo, alisema wanashukuru wameshirikishwa katika mchakato mzima wa kuhamishwa eneo hilo na amewaomba radhi abiria kwa usumbufu watakaoupata kwa kuwa ni moja ya mikakati ya serikali katika kurahisisha hali ya usafiri nchini.


Naye Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhinini (Latra) Mkoa wa Dar es Salaam, Rahim Kondo, amewataka madereva wa daladala za ruti zilizotajwa h kuheshimu maelekezo na kueleza kuwa hatarajii kuona zikikatisha ruti na kuleta usumbufu kwa abiria.


Mtendaji Kata ya Kivukoni, Aristides Balile, ameomba watumiaji wa vituo vilivyopaangwa kuhakikisha wanaheshimu maeneo hayo kwa kuwa ni maeneo maalum, ikiwemo kuepuka kuchafua mazingira kwa kuwa kutakuwepo na vifaa vya kutosha vya kuhifdhia taka.


Baadhi ya abiria wakizungumzia mabadiliko hayo, akiwemo Razia Amri alisema utamuongezea gharama za usafiri kwa kuwa awali alizoea kupanda gari moja kutoka Gongolamboto, sasa atalazimika kuchukua na bajaji ambayo nauli yake ni kati ya Sh500 hadi Sh1,000.


"Sisi tunaoenda kuchukua samaki kurudi kwa daladala Kivukoni kulitusaidia sana,sasa ni wazi tunaenda kubeba mizigo hii kichwani kwani itakuwa haitulipi," alisema Diana Ambrose mfanyabiashara wa samaki na mkazi wa Tabata Chang'ombe.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad