Diamond Platnumz Ahofia Kupata Hasara kwa Dvoice "Msanii Amechoka"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Diamond Platnumz Ahofia Kupata Hasara kwa Dvoice "Msanii Amechoka"

Msanii Diamond Platnumz ameonesha kuingiwa na wasiwasi wa kuanza kuchezea hasara baada ya kuwekeza hela ndefu katika usajili wa msanii wake mya, Dvoice Ginni.


Kupitia Instagram, kipande cha video kilipakiwa kikimuonyesha msanii huyo dogo akiwa amejilaza sakafuni katika hali ya uzembe huku bosi wake, Diamond Platnumz akizungumza baada ya kuingia chumbani na kumkuta amelala kizembe.


Diamond alianza kuzungumza katika kile ambacho kimechukuliwa na wengi kuwa ni utani kuwa ameanza kupata hofu huenda Dvoice hatoweza kurudisha faida ya kiasi cha pesa kilichowekezwa kwa usajili wake.


Diamond alianza kusema kwamba amepata wasiwasi huo baada ya kumuona msanii wake kalala sakafuni kwa mchoko wakati ambapo anahitajika kujitoa kimasomaso studioni kufanya miradi ya miziki ili kurejeshea lebo faida.


“Sasa huyu msanii ndugu, yangu, hebu imafine ndugu zangu na nyinyi mnisaidie, msanii ndio pale vile keshatoa EP na video mbili ndio huyu keshachoka kama hivi. Hebu nisaidieni sasa kama nyinyi mngekuwepo meneja au mwekezaji, hivi hela yangu inarudi hapa kweli jamani? Hela ipo kweli?” Diamond alimuuliza aliyekuwa anarekodi video hiyo huku wote wakicheka kwa utani.


Dvoice ametambulishwa katika lebo ya Wasafi kama sajili ya 7 tangu kuanziwa kwa lebo hiyo Februari 2016. Diamond Platnumz na uongozi wa lebo waliwekeza pakubwa na kutumia nguvu nyingi kumtambulisha Novemba 16, mpaka sasa ana mwezi mmoja chini ya lebo ya ameshatoa albamu yake lakini pia video mbili za ngoma.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad