Maskini Mzee Mwinyi Rais Mstaafu Augua Ghafla Alazwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Da es Salaam. Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na msemaji wa familia, Abdullah Ali Mwinyi imeeleza kuwa, Rais huyo mstaafu, anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye dua, swala na maombi, imesema taarifa hiyo iliyotolewa usiku huu.

"Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.

"Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali." taarifa hiyo imesema.

Mwinyi aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani katika utawala wa Julius Nyerere kisha akawa Rais wa Zanzibar na Rais wa awamu ya pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad