Mtoto wa Nyerere Aondoa Utata Kuhusu Sanamu "Yule ni Baba Yangu Kabisa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Serikali imesema imesikia sintofahamu na hisia tofauti kuhusu sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambayo imewekwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia na kuzinduliwa February 18, 2024 ambapo imesisitiza kuwa Mtoto wa Mwalimu Nyerere aitwaye Madaraka Nyerere ambaye alikuwa kwenye Kamati ya kuitengeneza sanamu hiyo, amesisitiza kuwa sanamu hiyo inafanana kabisa na Baba yake hivyo kama kuna Mtu anabisha amuulize yeye.

Akiongea leo Ikulu Dar es saam, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Balozi Shaibu Said Musa amenukuliwa akisema yafuatayo “Ni kweli kumekuwa na feeling na reaction ambazo wapo wanaosema kuna hitilafu lakini nataka mjue kwamba upande mmoja wana mawazo hayo lakini upande wa pili wapo wenye kukubali na kusema kwamba ni Mwalimu Nyerere, swali limeuliza, Serikali imelipokeaje?”

“Serikali imefuata maelezo ya kitaalamu yaliyotolewa na Kamati maalum ya Wataalamu ambayo ilishiriki mjadala na mpaka kupatikana kwa sanamu, sanamu ile ilifadhiliwa na SADC kwa wazo ambalo lilitokana na Viongozi wakiongozwa na Mugabe wakati wa uhai wake kuhusu namna ambavyo watamuenzi Mwalimu Nyerere, kama tunavyojua Tanzania chini ya Uongozi wa Mwalimu tulikuwa mstari wa mbele kuongoza mapambano ya Uhuru wa Afrika, SADC wakaona na AU kukubali liwekwe lile sanamu”

“Kamati ilihusisha Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Familia ya Mwalimu Nyerere akiwemo Madaraka Nyerere, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuanzia hatua ya awali mpaka hatua ya mwisho sanamu kukamilika Kamati iliridhika”

“Kamati iliridhika kwa vigezo gani?, cha kwanza Mwalimu mnayemuona katika sanamu ile ni Mwalimu anayeelezwa wa miaka ya 60 mpaka miaka ya 80 wakati yupo active katika mapambano ya kuleta Uhuru na maendeleo katika Nchi za Afrika, pili kauli ya Mwanae Madaraka Nyerere ameitoa mara kadhaa na mpaka siku ya uzinduzi nilikuwepo Addis ameendelea kusisitiza yule ni Baba yake na kama kuna anayebisha amuulize yeye na mkitaka kumuhoji mnaweza kumtafuta” amemalizia Naibu Waziri Balozi Shaibu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad