Diaara, Aziz Ki Watua kambini, Washudha Presha Yanga

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Diaara, Aziz Ki Watua kambini, Washudha Presha Yanga



Nyota wa Klabu ya Yanga, kiungo Stephanie Aziz Ki na kipa Djigui Diarra wametua kwenye kambi ya timu hiyo kuungana na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi.


Awali akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo, pamoja na majeraha waliopo kwenye kikosi chake, Kocha wa Yanga Miguel Gamondi alisema Aziz raia wa Burkina Faso na Diarra raia wa Mali hawajafika kambini licha ya kwamba aliamini wametua nchini alfajiri ya leo wakitokea kwenye majukumu ya timu zao za Taifa.


Aziz na Diarra wameshusha presha ya kocha Gamondi na mashabiki wa Yanga ambao walikua na wasiwasi itakuwaje kuwavaa Masandawana bila kuwa na wachezaji wao muhimu kwenye kikosi.


Yanga na Mamelodi watakipiga kesho Jumamosi katika Dimba la Mkapa majira ya saa 3 usiku.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad