Makonda Atoa Mpya Adai Anawajua Wanaomtukana Rais Mitandaoni Ikiwemo na Mawaziri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Paul Makonda
Paul Makonda

Monduli. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amedai anawafahamu baadhi ya watu wanaotuma watu kumchafua Rais Samia Suluhu Hassan mitandaoni na kwamba baadhi yao ni mawaziri.

Amesema endapo watu hao wataendelea kumchafua Rais Samia mitandaoni hadi kufikia Aprili 15, 2024, atawataja kwa majina.

Makonda ametoa madai hayo leo Aprili 12, 2024 mbele ya Rais Samia baadaya ibada maalumu ya kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Enguik, kata ya Monduli Juu wilayani Monduli, mkoani Arusha.


Makonda amesema watu hao wana lengo la kumkatisha tamaa Rais Samia katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa nchi, na kwamba miongoni mwa wanaofanya hivyo ni wale aliowapa nafasi za uongozi serikalini.

“Nitumie fursa hii kuwaambia hasa kaka zangu, mnaotuma na kuwalipa watu kumchokoza mama yangu, ninawajua na ninyi mnawajua, narudia tena hasa kaka zangu mnaotuma kulipa watu kumchokoza mama yangu Samia.

“Nawajua kwa majina na leo tarehe 12, nataka iwe mwisho kuwatuma watu kwenye mitandao ya kijamii kumtuka Rais Samia na Jumatatu ikiendelea natataja majina, wengine ni mawaziri,” amesema Makonda.

Pia, mkuu huyo wa mkoa wa Arusha amewataka viongozi wa dini kumwombea Rais Samia vizazi vijavyo vije kusoma hadithi nzuri za kiongozi huyo mwanamke ambaye ndiyo mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania.

“Naomba kukutia moyo, mimi nina mtoto wa kike na najua wengi wana watoto wa kike, wanatamani watoto wao wa kike, ikiwemo na mimi waje wasome hadithi njema za uongozi uliofanywa na kiongozi mwanamke na mahiri ambaye anaongoza Taifa hili.

“Ulinzi wa bunduki na watu wa usalama kwa taarifa unaweza usiuponye moyo, lakini neno la uzima linalotoka kwa watumishi wa Mungu linaweza kuponya moyo wako, nakuombea kwa Mwenyezi Mungu, akupe wigo na utakaolinda moyo wako, ili ututumikie sisi Watanzania,” amesema.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad