Mvua Zinazoendeea Kutibua Ratiba ya Michezo ya Ligi Kuu Bara.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Binti wa Kiislamu atandikwa bakora 100 kwa kuhudhuria kanisani« NyumaMbele »Comments (0)Listen to Article WhatsApp Facebook Twitter Email This Binti wa Kiislamu atandikwa bakora 100 kwa kuhudhuria kanisani Binti wa Kiislamu atandikwa bakora 100 kwa kuhudhuria kanisani Watu saba wa familia moja ya Kiislamu mashariki mwa Uganda wamekamatwa na mamlaka kwa madai ya kumpiga msichana wa miaka 18 ambaye alihudhuria ibada ya kanisa, polisi wamesema.  Msichana huyo anadaiwa kuchapwa viboko 100 na mjoma wake huku wajomba zake wengine watano wakimshikilia chini, tovuti ya habari ya Nile Post iliripoti.  Picha zilizoonekana kuonyesha msichana huyo akipigwa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, na kuzua hisia kali miongoni mwa Waganda.  Familia bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na tukio hilo.  Wajomba wa msichana huyo walikamatwa pamoja na shangazi yake, ambaye ni mlezi wake mkuu, polisi walisema.  Wataendelea kuzuiliwa wakisubiri uchunguzi, Samuel Semewo, kaimu msemaji wa polisi wa mkoa, alinukuliwa akisema.  Mwakilishi wa eneo hilo wa baraza la kitaifa la Waislamu alisema shambulio hilo ni la kinyama na haliungwi mkono na kanuni za dini, gazeti la Daily Monitor liliripoti.


Mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali hapa nchini, zimeonekana kutishia kutibua ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Bara.


Jumanne wiki hii, ilishuhudiwa mchezo baina ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga ukiahirishwa muda mfupi kabla ya kuanza kutokana na hali ya Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kutokuwa nzuri.


Uwanja huo uliopo Mbweni, Dar es Salaam, ulijaa maji hali iliyowalazimu wasimamizi wa mchezo huo kuuahirisha, ukapigwa kesho yake Jumatano na kumalizika kwa suluhu.


Licha ya uwanja huo kutumika, lakini Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alionekana kutoridhishwa na uamuzi huo akisema ilipaswa uahirishwe kwani uwanja haukuwa vizuri.


“Kupata alama moja kwenye Uwanja kama ule ni kitu kizuri tu kwangu, unawezaje kushinda kwenye uwanja kama ule? Sijui ni maamuzi gani haya yamefanyika,” alilalamika Gamondi.


“Huwezi kucheza mpira wa kuvutia kwenye Uwanja kama ule, tunaona soka la Tanzania linapiga hatua ni jambo zuri, lakini Uwanja kama huu unakwenda kuiweka wapi heshima hiyo, kwa nini ilazimishwe mechi kuchezwa pale ingekuwa sawa hata kusogeza mechi mbele au kuhamishwa kupelekwa Uwanja mwingine,” alisema Gamondi.


Ukiachana na Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, viwanja vingine ambavyo vipo hatarini zaidi kuathiriwa na mvua pindi ikinyesha kwa kiwango kikubwa ni Manungu uliopo Morogoro, CCM Kirumba (Mwanza), Sokoine (Mbeya) na Nyankumbu (Geita).


WENYE VIWANJA WANASEMAJE


Mwenyekiti wa JKT Tanzania ambao ni wamiliki wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Godwin Ekingo alisema wanachokifanya ni kutekeleza mambo yote ya msingi yanayohitajika ili uwanja wao uendelee kutumika katika kila mechi zao za nyumbani kwani fahari yao kubwa ni kucheza hapo.


“Mwanzoni tulikuwa tunatumia Uwanja wa CCM Kambarage kule Shinyanga kwa michezo yetu ya nyumbani ila baada ya kuonekana wetu wa Isamuhyo umekidhi vigezo tulirudi kwa ajili ya kuiweka timu yetu karibu na mashabiki wetu wanaotuzunguka,” alisema.


Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba, Lazaro Roman amesema kuna maboresho wameyafanya ambayo mvua ya kawaida ikinyesha mechi zinachezeka, lakini kama yakija mafuriko, hali itakuwa tete.


“Mechi ya Singida na Yanga mvua ilinyesha sana takribani saa tatu kabla ya mchezo kuanza lakini haikufanya mechi iahirishwe, uwanja wetu una mfumo wa kutoa maji uwanjani labda mvua iwe ya mafuriko ambayo hayawezi kuzuilika,” alisema Roman.


“Lakini kwa mvua hizi za kawaida bado uwanja wetu hauwezi kupata changamoto yoyote na kusababisha mechi kuahirishwa. Hata mechi iliyopita watu wengi walitegemea mechi ingeahirishwa lakini mechi haikuwa hivyo baada ya maji kuondoka uwanjani kwa haraka.”


KAULI YA BODI YA LIGI


Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Steven Mguto, alisema ni mapema sana kuzungumzia suala hilo ingawa wao wanachotambua viwanja vyote vilivyopitishwa vimekidhi matakwa na ndio maana vinatumika kwa michezo mbalimbali.


“Suala la kufungia kiwanja linatokana na kutokidhi kwa mahitaji yanayohitajika na tunapata taarifa kutoka kwa wakaguzi wetu, tutakuwa na kikao hivi karibuni, hivyo tutakapopata ripoti kutoka kwao ndipo tutachukua hatua,” alisema.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad