Mwanachuo Alieuawa Kwa Kuchomwa Kisu Hostel Azikwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mwanachuo Alieuawa Kwa Kuchomwa Kisu Hostel Azikwa

Mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Manispaa ya Morogoro, Hajrat Shaban aliyeuawa baada ya kuvamiwa akiwa kwenye hosteli za chuo na kuchomwa kisu amezikwa leo mkoani hapa.


Richard Mkesi ambaye ni mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro katika mazishi hayo amesema watahakikisha watuhumiwa waliohusika na mauaji ya mwanafunzi huyo wanakamatwa.


"Kama Jeshi la Polisi tuna wajibu wa kuhakikisha watu wote walioshiriki katika tukio hili wanakamatwa na wanachukuliwa hatua za kisheria,"amesema Mkesi.


Akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba huo Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Joseph, Julius Usiga amesema chuo kitamkumbuka Hajrat kwa uongozi wake katika Serikali ya wanafunzi.


"Marehemu atakumbukwa kwa kuwa alikuwa hodari na shupavu; katika maisha yake aliwaunganisha wanafunzi na uongozi wa chuo kwa jumla, alikuwa kiongozi wa Serikali ya wanafunzi na mpaka mauti yanamfika alikuwa Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi kwenye chuo chetu,"amesema Usiga.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad