TMA Yatoa Taarifa Mpya Kuhusu Hali ya Hewa, Mvua Kubwa Mikoa 26

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

TMA Yatoa Taarifa Mpya Kuhusu Hali ya Hewa, Mvua Kubwa Mikoa 26

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa na ngurumo kwa mikoa 26 ya Tanzania Bara na visiwa vya Unguja na Pemba kuanzia leo Aprili 22, 2024.


Mikoa ambayo inapata mvua leo Aprili 22, 2024 kwa mujibu wa TMA ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Dodoma, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe. Pia visiwa vya Unguja na Pemba.


Mwendesha bodaboda na watembea kwa miguu wakitafakari namna ya kukatisha katika eneo lililofurika maji jirani na stesheni ya mabasi yaendayo haraka (Udart), Jagwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha. Picha na Maktaba

“Angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya Mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba,” imeandikwa kwenye taarifa ya TMA ya matarajio ya hali mbaya ya hewa ya siku tano kuanzia jana Aprili 21, 2024.

Kwa siku ya leo angalizo la uwepo wa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa kufikia mita mbili, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Muonekano wa barabara katika eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam baada ya mvua kunyesha. Picha na Maktaba

Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani.

Aprili 23

TMA kupitia taarifa imesema Aprili 23, angalizo la mvua kubwa linatolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa kufikia mita mbili, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoo ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba),” imeeleza taarifa hiyo.

Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani

Aprili 24

Angalizo la mvua kubwa limetolewa katika maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia, angalizo la upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa Pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani

Aprili 25

Agalizo la mvua kubwa limetolewa katika Mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad