Waandishi wa Habari Waiba Vitu Katika Ndege ya Rais wa Marekani

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Waandishi wa Habari Waiba Vitu Katika Ndege ya Rais wa Marekani



Waandishi wa habari wametakiwa kuacha kuiba vitu kutoka ndani ya ndege ya Rais wa Marekani.

Hesabu ya vitu ndani ya ndege hiyo- Air Force One- baada ya ziara ya Joe Biden katika pwani ya magharibi ya Marekani mwezi Februari iligundua vitu kadhaa kutokuwepo katika eneo wanalokaa waandishi wa habari.

Foronya za mito, glasi za maji, na sahani za chakula ni miongoni mwa vitu vinavyodaiwa kuchukuliwa kutoka ndani ya ndege hiyo.

Chama cha waandishi wa habari wa Ikulu ya Marekani kimeonya kuwa uchukuaji wa vitu ndani ya ndege hiyo ni marufuku.

Mwezi uliopita chama hicho kilituma barua pepe kwa waandishi na kusema tabia hiyo inaleta picha mbaya kwa waandishi ambao husafiri na rais na tabia hiyo ikome mara moja.

Waandishi mara nyingine hupewa paketi ndogo za chokleti zikiwa na nembo ya rais kama kumbukumbu.

Lakini kuchukua vitu vyenye nembo ya Air Force One, ikiwemo vijiko na taulo, ni jambo ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka mingi, taarifa zinasema.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad