Mambo Matano Yaliyoipa Ubingwa wa Ligi Kuu Yanga Haya Hapa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

KILICHOBAKI kwa Yanga ni sherehe tu za ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao imeutwaa Mei 13 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 3-1, huku pia ikiwa na hesabu za kubeba Kombe la Shirikisho (FA) ambalo ipo katika nusu fainali itakayocheza Mei 19 dhidi ya Ihefu.

Mashabiki wa Yanga kwa sasa wanatembea vifua mbele huku wakiwatambia wenzao wa Simba kwa kubeba ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo ukiwa ni wa kwanza chini ya kocha Miguel Gamondi ambaye amewafanya msimu huu kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Baada ya kumalizana na Ihefu katika kombe la FA, Yanga itakuwa ikipewa heshima yake katika michezo mitatu iliyosalia katika ligi kwa kupiga 'parade' dhidi ya Dodoma Jiji (ugenini) huku miwili ya mwisho ikiwa nyumbani dhidi ya Tabora United na Mfaande wa Tanzania Prisons.

Katika michezo mitatu iliyosalia Gamondi ambaye ameiongoza Yanga kufikisha pointi 71 atakuwa akifukuzia rekodi ya Nasreddine Nabi ambaye aliipa timu hiyo ubingwa wa ligi msimu uliopita 2023/23 ikiwa na pointi 78, anaweza kufikia na kuvunja rekodi hiyo ikiwa atavuna pointi tisa za michezo hiyo.

Yapo mengi ya kuongealea kuhusu Yanga lakini haya ni mambo matano ambayo yameibeba timu hiyo ya Wananchi yenye maskani yake Jangwani na kuweka historia ya kutwaa ubingwa wa 30 tangu kuanzishwa kwake miaka 89 iliyopita.

MABAO YAMETAWANYWA
Yeyote anaweza kukuadhibu hivyo imekuwa ngumu kwa Yanga hii ya Gamondi kutabirika tofauti na msimu uliopita ambapo alikuwa akitegemewa kwa kiasi kikubwa Fiston Mayele katika upachikaji wa mabao.

Pamoja na Gamondi kuwa na washambuliaji wa kati kiasili Clement Mzize, Joseph Guede na Kennedy Musonda wenye mabao 14 kwa pamoja, lakini amebebwa zaidi na safu ya kiungo ikiongozwa na Stephane Aziz KI aliyefunga 15, Max Nzengeli, Mudathiri Yahya wenye mabao tisa na Pacome Zouzoua mwenye saba.

Kwa upande wa ukuta wao, mabeki wa pembeni, Kouassi Attohoula 'Yao' ana asisti saba (kinara kwa mabeki), Nickson Kibabage akiwa nazo nne huku mabeki wao wa kati, Dickson Job na Bakari Mamnyeto kila mmoja amacheka na nyavu mara moja mbali na kuwa na jukumu mama la kulinda.


UKUTA CHUMA
Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson aliwahi kusema kuwa mabeki wanashinda mataji lakini washambuliaji hushinda mechi, alikuwa na maana kwamba mchango wa mabeki katika kufanikisha mpango wa kutwaa ubingwa ni mkubwa na hilo limejidhihirisha kwa Yanga.

Ukuta wa Yanga unaoundwa na kipa, Djigui Diarra na mabeki, Yao, Joyce Lomalisa, Kibabage, Kibwana Shomary, Ibrahim Hamad 'Bacca', Mwamnyeto, Gift Fred ambao kila mmoja alitumika kwa nafasi yake wameisaidia timu hiyo kuwa salama. Yanga ndio timu iliyoruhusu mabao machache zaidi (13).

Akiongelea namna ambavyo mabeki wa Yanga wamefanya kazi kubwa msimu huu, nyota wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema, "Kama ni makosa ambayo yalionekana ni madodomadogo lakini kwa ujumla wamefanya vizuri, Hamad, Job na hata Mwamnyeto wameitendea haki beki ya kati."


UPANA WA KIKOSI
Kipindi ambacho makocha wengine walikuwa wakipata wakati mgumu kutokana na idadi kubwa ya mechi ambazo walikuwa nazo katika ratiba zao kwa kipindi kifupi, Gamondi alikuwa akipeta huku akifanya mabadiliko kadhaa ambayo yalikuwa yakimbeba ili kutoa nafasi kwa wengine kupumzika.

Mfano mzuri ni ndani ya April ambapo Yanga ilikuwa na michezo sita ya mashindano matatu tofauti, Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilikuwa mchezo wa marudiano dhidi ya Mamelodi Sundowns, Kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji na Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida FG, Simba, JK Tanzania na Coastal Union.

Ndani ya michezo hiyo, Yanga haijapoteza katika dakika 90, iliondolewa na Mamelod kwa mikwaju ya penalti, iliifunga Dodoma Jiji katika Kombe la FA kwa mabao 2-0 huku ikivuna pointi 10 kati ya 12 katika michezo minne mfululizo ya ligi, alimudu kufanya yote hayo bila ya Pacome na hata Yao ambao walipata majeraha Machi katika mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC.

MECHI KUBWA
Kupata ushindi dhidi ya wapinzani wako ambao wanawania nao ubingwa wa ligi ni miongoni mwa mambo muhimu kufanywa na timu ambayo inahitaji ubingwa, Yanga imelifanya hilo.

Msimu huu, Yanga imevuna pointi sita mbele ya Simba na mabao saba, imevuna pointi tatu mbele ya Azam kwa kuwafunga mara moja katika mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa mabao 3-2, matajiri hao wa Chamazi walijitutumia katika mzunguko wa pili na kulipa kisasi kwa kushinda kwa mabao 2-1.

Hata hivyo Yanga msimu huu, imeweka rekodi ya kuzifunga timu zote 15 katika ligi, kama kuna ambao walipona katika mzunguko wa kwanza basi katika mzunguko wa pili walikumbana na kipigo mfano mzuri ni Kagera Sugar ambao mchezo wa kwanza walitoa suluhu lakini walipokutana kwa mara nyingine tena walitandika kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

BENCHI LA UFUNDI
Ikiwa hakuna utulivu katika benchi la ufundi ni ngumu kwa timu kufikia malengo yake. Utulivu wa Gamondi na ushirikiano kwa wenzake wa benchi la ufundi ni miongini mwa mambao ambayo yameibeba Yanga kwa kiasi kikubwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya 30.

Kivipi? Achana na mbinu za Gamondi ndani ya uwanja na namna ambavyo amekuwa akikiandaa kikosi, wakati mchezo ukiendelea yupo, Mpho Maruping ambaye ni mtaalam wa kuchambua 'video analist' hufuatilia na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na benchi hilo la ufundi.

Msauzi huyo huwa na kifaa maalum ambacho humsaidia kufanya mawasiliano na meneja, Walter Harrison kwa lengo la kushauri kutokana na mwenendo wa mechi kwa takwimu zake, ujumbe wake hufikishwa kwa Gamondi.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad