Luis Miquissone Mchezaji Anaelipwa Mshahara Mkubwa Kuliko WOTE Simba Aleta Mgawanyiko Mkubwa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Luis Miquissone Mchezaji Anaelipwa Mshahara Mkubwa Kuliko WOTE Simba Aleta Mgawanyiko Mkubwa


HATMA ya Kiungo Mshambuliaji wa Simba anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo,  Luis Miquissone ipo mikononi mwa Uongoozi wa timu  hiyo.

Wakati huu  wa usajili wa  dirisha kubwa,  ambalo pia uhusisha na taarifa za baadhi ya wachezaji kutemwa kwenye timu zao, kwa kuvunjiwa mikataba au kuuzwa na kuachwa huru, kesi hii huenda ikamkuta nyota huyo ambaye kwa msimu uliomalizika  hakuwa na kiwango kizuri.

Simba inaendelea kujipanga zaidi, huku ikiangali namna ya kuachana na nyota wake ambao hawakuwa na wakati mzuri uwanjani,  licha ya kupatiwa nfasi ya kuonesha uwezo.

Moja kati ya wachezaji ambao ameleta mgawanyiko na makundi sio tu kwa mashabiki bali hata kwenye Uongozi, juu ya hatma   yake ni Luis Miquissone aachwe au aendelee kwa msimu uliobakia, lakini je akivunjiwa mkataba gharama zake zikoje? endelea kusalia nasi…

Luis Miquissone wakati   anarejea Simba alisaini mkataba wa miaka miwili,hivyo hadi sasa amebakiza mwaka mmoja,rasmi atakuwa huru june 30/2025.

Miquissone ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote Simba na ni miongoni mwa wachezaji wawili wanaolipwa hela nyingi ligi kuu bara. Kiasi cha Tsh m47.


Pia kwenye mkataba wake kuna bonasi mbalimbali mfano akifunga goli anapewa $200 na akitoa pasi ya goli anapewa $100 ila kwa bahati mbaya hakuwa na msimu mzuri.


Kubwa zaidi kwenye mkataba wa Luis Miquissone na Simba kuna kipengele cha kuvunja mkataba huo mwishoni mwa simu huu endapo Simba hawatoridhishwa na kiwango chake.


Na mkataba huo ukivunjwa Simba hawatatakiwa kumlipa chochote.


Hivyo hatima ya Luis Miquissone iko mikononi mwa viongozi wa Simba.


Kwenye jambo  hili viongozi wa Simba wanastahili sifa na pongezi walicheza kama Chama anapokuwa ndani ya boksi la  mpinzani huwa anatulia,  Kipengele hiki kinawaweka Simba sehemu salama endapo  wataamua kumvunjia mkataba Luis hawata ingia gharama ya kumlipa fidia.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad