Tundu Lissu : Kuna Watu Wananifuatilia na GARI Kwenye Mikutano yangu

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Tundu Lissu : Kuna Watu Wananifuatilia na GARI Kwenye Mikutano yangu


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema tangu ameanza ziara yake kuna gari inafuatilia msafara wake na wakifika kwenye mkutano Watu hao hujificha hali ambayo inamuogopesha hivyo ameomba kama Watu hao ni Polisi wamuambie ili awe na amani na wasiposema kesho atawanyooshea vidole kwenye mkutano.


Tundu Lissu amesema hayo wakati akiwa kwenye mkutano katika Kata ya Matumbo Jimbo la Singida Kaskazini.


“Toka nimeanza ziara yangu kuna gari inatufuatilia halafu wakifika kwenye mikutano wanajificha, nyinyi mnajua mimi nimeshambuliwa sasa nikiona hali kama hiyi ninaogopa, nataka niseme kama ni Polisi mje mniambie kama mmetumwa na Serikali niambieni ili niwe na amani msiposema kesho kwenye mkutano wangu nitawanyooshea kidole ili Wananchi wawatambuwe kama ni Wakazi wa sehemu husika maana Vijana wangu wameshawatambua”


Itakumbukwa Mwezi August mwaka 2017 Tundu Lissu aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari na kusema kuna Vijana wanamfuatilia kila anapokwenda, na baadaye September 17,2017 Lissu akashambuliwa kwa risasi akiwa Jijini Dodoma.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad