Gossip, Politics And Love Affairs

Isha Mashauzi Classic Akiri Kutumia Madawa ya Kulevya Kabla ya Kupanda Jukwaani

STAA wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya mirungi

Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika maisha yake ya kawaida nje ya usanii.

Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.Tupe Maoni Yako

Post a Comment

eeeh nyie waandishi kboko duuh mtu ukisoma kchwa cha habari unaweza ukazimia hlf unakuta hbr yenyewe cheche tupu!! tupunguzen kupotosha jamii jaman

acheni kuandika pumba juu ya mtu madawa madawa au nyinyini ndio mnatumia nini

Yaan polisi nao wamesimama kama mashoga juzi mmenikamata na GOMBA langu sasa isha huyo kajianika anatumia nendeni mkamkamate wala rushwa nyie.....LAMAMAEEE!!!!

[blogger]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget