Aibu-Baada ya mahojiano Makosa yaliyomnyima Lema Dhamana ni Haya kwa mujibu wa mwanasheria wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jioni hii ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Sasa haya maneno hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane na kuzua taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka sheria

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

Sasa hayo waliyoita makosa ya uchochezi ndiyo yaliyomnyima haki ya dhamana leo.tutafakari kama Arusha itatawalika kwa hali hii.

Hebu tupime makosa hayo matatu kama yanaweza ku-justfy mambo yote yaliyotokea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie CCM Hakuna anaeweza kuizuia kweli kwani kweli huishi daima.. kwataarifa yenu kila mnavyoendeleza uonevu kwa raia na kwa viongozi wa upinzani ndivyo ambavyo mnapoteza mvuto na kuwapalilia njia CHADEMA kuelekea ikulu.. ViVA CHADEMA..

    ReplyDelete
  2. KASUMBA NI UGONJWA MBAYA KUPITA UKOLONI

    ReplyDelete
  3. Hakuna uchochezi wowote,ni ukweli mtupu,sema hatupendi kuambiwa ukweli,jamani hapo AR mjini kunani nyie CCM,mmetuchosha na siasa zenu za maji taka

    ReplyDelete
  4. Lema ana psychological problem. Inawezekana malezi ya utotoni mwake ndio yanatoa majibu sasa. So people take an extra miles kufikiria mnapokua na huyu bin adamu.

    ReplyDelete
  5. Huyu jamaa aliyekomenti hapa juu hana akili, kichwani amebeba mavi za mafisadi jambo linalonifanya kutoshangaa kuona upuuzi kama huu ukiandikwa

    ReplyDelete
  6. The stupidity of our leaders brought us here we are, The Tanzanians of today understand much about CCM's politics that is full of non visioned people, old version that are no longer needed in the digital world. It doesn't mean that they know nothing, they are preparing their life and life of their children, friends and relative as they will soon sell all the territory and all on it as well as Tanzanians to white men. Up to the moment we Tanzanians posses only air that we inhel for free that may soon be being charged.

    ReplyDelete

Top Post Ad