Wafu wanavyofukuliwa, kisha kuzikwa wapya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siku zote tunaamini kuwa mtu anapofariki hupumzika kwa amani, lakini siku hizi wafu hao hawapumziki tena kwa amani, bali huamshwa, kisha, wafu wengine kushika nafasi zao.

Ni kama vile muda wa marehemu hao kukaa kaburini umekwisha hivyo, nafasi zao zinatakiwa kutumiwa na wengine kutokana na uhaba wa maeneo ya kuzikia.

Maeneo mengi ya kuzikia katika Jiji la Dar es Salaam, hasa yale maarufu kama Kinondoni, Sinza, Temeke na Kisutu yanapendwa zaidi na watu na sasa yamefurika.

Kujaa kwa maeneo haya ya kuzikia kumesababisha makaburi ya watu wengine, kufukuliwa kisha kutumika kuzikia miili mingine.

Hata hivyo, makaburi ambayo hufukuliwa ni yale ambayo hayajajengewa, yametelekezwa, hayana kitu chochote cha kuonyesha kuwa kuna kaburi pale au mengine hayana alama kama misalaba au imeondolewa.

Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Kaiohela anasema kuwa anafahamu kwamba makaburi hayo yamejaa, lakini hakutaka kuzungumza zaidi akitoa ahadi kuwa siku ya Jumatatu atalifikisha suala hilo kwa wahusika wakuu.

Katika makaburi ya Temeke Chang’ombe, Mwananchi Jumapili lilishuhudia makaburi yakiwa yamesongamana kiasi ambacho ni vigumu mtu kupata nafasi ya kuweka mguu.

Mlinzi wa makaburi hayo, Athuman Mtembwe anasema kutokana na ufinyu wa nafasi katika makaburi hayo, makaburi ambayo hayana alama yoyote ni rahisi kufukuliwa na kuzikiwa kwa mara nyingine.

“Mimi kama mlinzi wa eneo hili ninaweza kukutafutia sehemu ambayo unaweza kuchimba kaburi, lakini kama hufahamu utafukua tu maiti nyingine,” anasema

Anasema kuwa mara kwa mara watu wanaokuja kuchimba makaburi ili kuzika ndugu zao, wamekuwa wakifukua miili ya watu wengine ambayo makaburi yao hayakuwa na alama yoyote.

“Ni kawaida, mchimba kaburi anafukua, anakuta mifupa, anaiweka pembeni au anaizika katika shimo dogo…kisha anaendelea na taratibu za kuzika mwili mwingine,” anaeleza.

Lakini Mtembwe anasisitiza kuwa iwapo atachimba yeye, hawezi kufukua kaburi lililokwishatumika kwani anafahamu maeneo machache ambayo hayajatumika, ingawa ni finyu mno.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wangeanza kuruhusu kaburi moja zaidi ya mtu mmoja kama ndugu linafukuliwa mtu anawekwa juu ya ndugu yake au jamaa, ndio maana ulaya utaona mabango yao na majina mengi wanawaweka side by side, au above, shimo moja mara nyingi hadi watu wanne wanazikwa.

    inasikitika kufukua kaburi la mtu mwingine, imagine ma ghost yanakutana na labda hayapatani.

    ReplyDelete

Top Post Ad