Lady Jay Dee Kufikishwa Kizimbani leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWANAMUZIKI nyota wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ Leo (Jumatatu) anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni  kufuatia taarifa alizofikishiwa Meneja na mume wa msanii huyo, Gadna G Habash ‘Captain’.
Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa Lady Jaydee kufika Mahakama ya Kinondoni, leo (Jumatatu) Mei 13, mwaka huu.

“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, hii ni baada ya kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo jana na kuleta barua ya kumkabidhi Lady Jaydee mwenyewe japo hawakumkuta” alisema Gadna.


Katika ukurasa wa Twitter wa Lady Jaydee saa tatu zilizopita aliandika hivi "Sumu ya teja Ukonga, Keko, Segerea. Kesho Mahakamani kizibiti ubaoniii eeeh aaah!" wakati siku ya Ijumaa katika ukurasa wake wa Facebook aliandika hivi:

"Ratiba ya usiku wa leo ni MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni... Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea... Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk asubuhi."
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole sana sister bado watu wanakufatilia
    wahenga wanasema maisha ni safari ndefu komaa dada

    ReplyDelete
  2. sijui kwanini ila nahisi jide anakosea sana

    ReplyDelete
  3. anakosea nn funguka au umetumwa

    ReplyDelete
  4. Yuko Sawa anapigania haki Yake,tuache kuridhika kwa peremende,kuna mengi yaliyojificha

    ReplyDelete
  5. Lengo la kwenda mahakamani ni kumzuia asiongee tena...alihadi kuelezea upande wake tar 15. Nini jamaa hawataki wananchi wajue???

    ReplyDelete

Top Post Ad