Mama Flora Mvungi Apiga Marufuku Sherehe ya Kibao Kata kwa Mwanae

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAMA mzazi wa msanii wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi, Zuhura Mvungi amepiga marufuku sherehe ya kibaokata cha mwanaye huyo na kudai kuwa ni ufuska hivyo kama kitafanyika basi ataigomea ndoa.
Kikizungumza na Amani, chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu wa Flora kilisema sherehe hiyo ilitarajiwa kufanyika Jumamosi iliyopita nyumbani kwa msanii Salma Jabu ‘Nisha’ Kijitonyama, Dar, lakini haikufanyika kutokana na mama Flora kukataa na kudai ni ufuska na ni kinyume na maadili ya Mtanzania.
“Kila kitu kilikuwa kimeshaandaliwa lakini mama Flora akamkataza mwanaye huyo kuwa hana ruhusa ya kufanya kwa sababu hivyo ni vitendo vya ufuska na siyo utamaduni wetu,” kilisema.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Flora na kumuuliza kulikoni?
“Mama alikataa nisifanyiwe kibaokata akidai ni ufuska hivyo anataka nifanye vitu ambavyo vinaendana na maadili,” alisema Flora.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad