Safari, Marando, Lema, Zitto kuwasha moto Bagamoyo leo jioni!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Viongozi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani na baadhi ya wabunge wa CHADEMA watafanya mkutano mkubwa wa siasa jioni ya leo tarehe -25/5/2013 (jumamosi) katika viwanja vya TOP TOP (karibu na stendi kuu ya BAGAMOYO)..

Mkutano huu unatarajiwa kuwa utakuwa mkutano mkubwa kuliko yote iliyowahi kufanyika kwa miaka 10 iliyopita. Ni mkutano ulioandaliwa vizuri kuliko mikutano mingine iliyopita. Vifaa vya kisasa vya uenezi na mawasiliano vitatumika.

Tunatarajia kupokea wageni zaidi ya 100 ambao watashiriki semina, kuendesha mkutano na vikao na watu wa rika na jinsia mbalimbali. Vikao vitaanza saa 3 asubuhi. Tumeishapokea wageni 53 mpaka saa 4 usiku wa kuamkia leo.

Wakazi wa Bagamoyo, wameonekana wakifurahia ujio wa viongozi wa CHADEMA na magari ya matangazo na mikutano. Viongozi wa wilaya zote za Dar es Salaam na Pwani watakuwepo..

Viongozi wa jimbo la Chalinze, Jimbo la Bagamoyo, Wilaya ya Bagamoyo na mkoa wa PWANI wote wako BAGAMOYO kwa kazi hii ya mkutano na kupokea wageni wetu..

Mkutano huo utaanza saa 8 mchana na kuisha saa 12 jioni. Mgeni rasmi atakuwa Prof. Abdallah Safari. Wageni wengine ni Mabere Nyaucho Marando, Zitto kabwe (ambaye jana alikuwa Lushoto) na Mh. Godbless Lema (ambaye jana alikuwa Muheza, Tanga)..

Mwenyekiti (w) Bagamoyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad