KAHABA LANASWA LIKIFANYA NGONO KATIKA MAKABURI YA MALAPA BUGURUNI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

LICHA ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watu wengi kuogopa kufanya maovu, jimama anayekwenda kwa jina la Joyce Benson (34), amefumwa akifanya ngono katika makaburi ya Malapa, Buguruni jijini Dar.

Joyce amekamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita saa nane katika maeneo hayo akifanya biashara haramu ya kuuza mwili wake katika makaburi hayo kwa njia ya kujipatia fedha.
 

Joyce mwenye umbile la miraba minne alipatwa na fedheha kubwa baada ya majirani zake kusikia habari hizo na kuanza kumlaani.

Mbali na Joyce pia siku hiyo machangudoa wengine 14, waliokuwa wakifanyia vitendo vya ukahaba kwenye makaburi hayo walikamatwa.

Joyce na wenzake hao walifikishwa katika Mahakama ya Jiji (Sokoine Drive) ili sheria ifuate mkondo wake.

Wakiwa mahakamani hapo, mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi aliwasomea tuhuma za kufanya ukahaba na kumfanya hakimu wa mahakama hiyo, Timoth Lyon kupigwa na butwaa.

Hata hivyo, Joyce na wenzake walikana kufanya kosa hilo ambapo hakimu, Lyon aliwaambia washitakiwa kuwa dhamana iko wazi kama watatimiza masharti.

Licha ya dhamana kuwa wazi, jimama huyo alijikuta akipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea baada ya kukosa mdhamini huku baadhi wakichomolewa na wadhamini wao. 

-GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swali walikutwa wanazini au? kama walikutwa wanazini wanaume waliokuwa wanazini nao wako wapi? Kama hawapo tunaweza tukasema sio haki?

    ReplyDelete
  2. Emmanuel Mgana27 July 2013 at 07:42

    Hawana hatia yoyote, ni ubabaishaji tu ni kuiongezea mzigo serikali kuwalisha Chakula huko Segerea, Wanaacha kushughulikia Mafisadi, majambazi, vibaka wanawasumbua hao wadada, hiyo ni miili yao wenyewe, haya hao wanamme mbona hatusikii wakamatwe na wao mbona washirika.

    ReplyDelete

Top Post Ad