NIFANYAJE BABA YANGU AJUE KUWA MIMI NI MTOTO WAKE?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sijui kama mtanielewa ila nataka nieleweke hata kwa kutumia akili za mwisho mlizo zaliwa nazo.

Mimi ni mtu mzima of course najua mema na mabaya na kwa upeo wangu leo hii ninatamani kujiweka huru ili nafsi iwe huru asilani.

Najijua kwamba baba aliyenilea sio baba yangu mzazi, lkn pia sitokuwa na moyo wa shukurani nisipomshukuru kwa moyo wa upendo na wa kujali wa baba aliyenilea. ukweli sijawah kujuta kulelewa nae na wala sijawah kuona tofauti kati yangu na watoto aliowazaa yeye. kanisomesha toka std 1 hadi elimu ya juu, kaniozesha kwa heshima zote na bado kanipa zawadi za kuanzia maisha mimi na hubby wangu. Ukweli najivunia kuwa naye as baba na naitwa kwa jina lake.

Wapendwa wangu kama mjuavyo damu nzito kuliko maji katika kukua kwangu wapambe (of which hawakosekanagi ) walinipa ukweli juu ya baba yangu mzazi. sijawah kumwona kwa macho ingawa namwona kwenye tv na magazeti tu. Mbaya zaid huyu baba sina uhakika kama alishawah kunitolea hata sh kumi ya matumiz lkn nimejikuta nafsi yangu ikitaka tu huyu baba ajue kwamba mm ni mwanae. kumwambia mama naogopa as nitamuumiza ama pia naweza kumuumiza baba. lakin nafsi inanisukuma sana nimtafute nimwambie ukweli.

sasa ishu inakuja hivi kwanza nitawezaje kumwambia huyu baba aniamini kwamba ni kweli?? wengi husema nimefanana naye usoni lkn sijui sana as najiona kama nimefanana na mama. kwa status yake pia naogopa isije ikawa headlines kwenye news ikamchafulia hadhi yake manake ni waziri fulan kwenye hii serikali.

on the other hand hivi nitakuwa nimemuumiza vipi mama yangu kwa kumwambia huyu baba ukweli?? je baba mlezi atachukulia poa ama ndio nitakuwa nimemkwaza?? ikumbukwe kwamba kanilea toka niko kachanga hadi leo hii na sijawah kujuta kwa yy kunilea.

naomba ushauri wako wa busara na sio matusi ama kashfa.

Source:Jamii forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eti unamuona kwenye magazeti ila wengne muwe mnatumia akili utoto wote usimjue uje ujulikane ukubwani? Huyo mpambe wake mtakuja umbuka kisa labda mama alikua anatoka na huyo wazr na mume wake at the same time so kumwadithia shoga age akaona hyo na baba ake. Dada jipange fsnya yako ksbisa utamwaibisha yy ila ww ndo utaibika. Pole samaki

    ReplyDelete

Top Post Ad