OFISA USALAMA "FEKI" ANASWA NA JESHI LA POLISI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.

Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.

Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.

Katika tukio jingine, jeshi hilo linawashikilia watu saba wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha, sare za polisi na simu za upepo.

Kova alisema tukio hilo lilitokea saa tatu asubuhi eneo la Kiluvya wilayani Kinondoni ambako watuhumiwa walikuwa wakitumia gari lenye namba za usajili T 546 BWR Toyota Cresta GX100 yenye rangi nyeupe.

Alisema baada ya watuhumiwa hao kuona wamezingirwa, walianza kufyatua risasi hewani, lakini polisi walipambana na kuwakamata.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Khamis Mkalikwa (40) mkazi wa Mbagala, Magira Werema (31) mkazi wa Mabibo na Nurdini Bakari (46) mkazi wa Temeke.

Wengine ni Materu Marko (32) mkazi wa Mbweni, Louis Omagoda (34) mkazi wa Kimara Kona, Amosi Enorck (23) mkazi wa Tegete Kibaoni na Amiri Mohamedi (45) mkazi wa Magomeni Mikumi.

Kova alisema baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walikutwa na bastola moja aina ya Brown B.3901 ambayo ilikuwa na risasi nne na ganda moja la risasi, sare za polisi pea mbili za cheo cha station surgeant (major), moja ya pea ikiwa ina beji inayosomeka kwa jina la SSGT A. M. Mduvike.

Watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa kwa mahojiano huku wengine wawili wakipelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa sehemu za miguu wakati wakikamatwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad