WACHEZAJI WATANO KUTOKA AFRICA WATAKAOCHEZA LIGI YA NBA 2013/2014

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



NBA Hasheem_Thabeet
Hasheem Thabeet (Tanzania)
Ndio mchezaji mrefu kuliko wote kwenye ligi ya NBA kwa sasa, majuzi wakati timu yake ya Oklahoma City Thunder ikicheza na Charlotte Bobcats Hasheem alicheza vizuri akiwa na point 13 alizofunga pamoja na kudaka Rebounds 10, huu utakua msimu wake wa pili akiwa na OKC.
NBA Gorgui_DiengGorgui Dieng (Senegal)
Dieng (23) amesajiliwa na Minnesota Timberwolves baada ya kufanya vizuri akiwa na timu ya Louisville Cardinals inayoshiriki ligi ya vyuo vikuu Marekani NCAA.
NBA Ike_DioguIke Diogu (Nigeria)
Ike ni mchezaji wa kiafrika ambae amewahi kucheza ligi ya NBA kwa muda mfupi kabla ya kwenda barani Asia alikochezea timu ya XINJIANG FLYING TIGERS, GUANGDONG SOUTHERN TIGERS na timu mbili za PUERTO RICO ambazo ni CAPITANES DE ARECIBOna LEONES DE PONCE ila kwa sasa anarejea kwa mara ya pili kwenye ligi ya NBA ambapo atachezea timu ya NEW YORK KNICKS.
NBA Bismack_BiyomboBismack Biyombo (DRC)
Unaambiwa moja ya majina makubwa kwenye mchakato wa kuchagua wachezaji wanaotoka vyuoni mwaka 2011 lilikua jina la Bismack Biyombo ambae alichaguliwa na timu ya SACRAMENTO KINGS na mwaka huu amesajiliwa na CHARLOTTE BOBCATS ambako atakua akishindana kutafuta namba na Cody Zeller aliyejiunga na timu hiyo msimu huu.
BASKETBALL-SENEGAL-ANGOLA-FINALCarlos Morais (Angola)
Carlos Morais amesajiliwa kuichezea TORONTO RAPTORS msimu huu akiwa na uzoefu wa kuiongoza Angola kwenye mashindano kadhaa ya kimataifa na amewahi kucheza kwenye mashindano ya FIBA Afrika 2005 na 2007, mashindano ya dunia mwaka 2006 pamoja na mashindano ya Olimpiki mwaka 2008.
Source: Millardayo.com

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. There are many Africans who play in the NBA, more than five. Please do your research.

    ReplyDelete

Top Post Ad